title : TatuMzuka yazindua ‘jackpots’ mbili kubwa za kubadili maisha kila wiki
kiungo : TatuMzuka yazindua ‘jackpots’ mbili kubwa za kubadili maisha kila wiki
TatuMzuka yazindua ‘jackpots’ mbili kubwa za kubadili maisha kila wiki
Wiki hii TatuMzuka imezindua jackpot ya Jumatano ikiwa ni jackpot ya pili ndani ya wiki moja. Watanzania sasa watapata fursa ya kuwa washindi wa jackpots mara mbili na hivyo kutengeneza washindi wengi zaidi kupitia jackpots.Jackpot ya jumatano ambayo itahusisha wachezaji wote waliocheza tangu jumapili itakuwa inaonyeshwa saa 3 usiku kupitia Clouds TV na EATV. 

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni hiyo, Bwana Sebastian Maganga alisema kampuni ya The Network ambao ni wamiliki wa mchezo wa namba wa TatuMzuka imekuwa ikiangalia namna ya kuongeza nafasi za Watanzania kushinda kwa wingi na kwa kiasi ambacho kinabadilisha maisha yao.
“Tangu tulipoanza mwaka mmoja uliopita tumetoa jackpot ya kihistoria ya milioni 300, na sasa kwa kuongeza jackpot ya jumatano watanzania hawatahitaji kusubiri wiki nzima kushinda, itakuwa sasa jumatano na jumapili” Alisisitiza Maganga
Baada ya uzinduzi huu, Tatumzuka sasa itaondoa jackpot ya kila siku ya Mzuka Deile na kuibadilisha na droo za vipindi maalumu ndani ya siku moja. Droo hizi zitatengeneza mamilionea wengi kwa haraka na kuufanya TatuMzuka kuwa mchezo unaotengeneza mamilionea wengi zaidi kuliko mchezo mwingine katika soko.

“Kwa tiketi moja ya shilingi 500 sasa Watanzania watakuwa wanasubiri kwa siku 3 tu kushinda kupitia jackpot za jumatano na jumapili. Hii itakata kiu ya wachezaji wetu wapendwa ya kusubiri muda mrefu kushinda kiasi kikubwa” Aliongeza Hussein
Ili kuongeza nafasi ya watanzania wengi kutazama shoo za jackpots Bwana Maganga alisisitiza kwamba The Network imeiongeza TBC1 kati ya vituo vitakavyokuwa vinaonyesha mubashara shoo ya jackpot ya jumapili.
Hivyo makala TatuMzuka yazindua ‘jackpots’ mbili kubwa za kubadili maisha kila wiki
yaani makala yote TatuMzuka yazindua ‘jackpots’ mbili kubwa za kubadili maisha kila wiki Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TatuMzuka yazindua ‘jackpots’ mbili kubwa za kubadili maisha kila wiki mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/tatumzuka-yazindua-jackpots-mbili-kubwa.html
0 Response to "TatuMzuka yazindua ‘jackpots’ mbili kubwa za kubadili maisha kila wiki"
Post a Comment