title : Shule za sekondari za Jeshi zazindua michezo ya mpira miguu
kiungo : Shule za sekondari za Jeshi zazindua michezo ya mpira miguu
Shule za sekondari za Jeshi zazindua michezo ya mpira miguu
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa( JKT )
Meja Jenerali Martin Busungu,akikagua timu za shule za shule sekondari katika ufunguzi wa michezo ya mpira miguu shule,zinazomilikiwa na JWTZ uwanja wa Uhuru Dar es Salaam leo (Picha na Heri shaaban)
Wanafunzi wa shule za sekondari za Jeshi wakiwa katika maandamano ya ufunguzi wa michezo ya shule,zinazomilikiwa na JWTZ uwanja wa Uhuru Dar es Salaam leo Picha na Heri shaaba)
Wanafunzi wa shule za sekondari za Jeshi wakiwa katika maandamano ya ufunguzi wa michezo ya shule,zinazomilikiwa na JWTZ uwanja wa Uhuru Dar es Salaam leo Picha na Heri shaaba)
Na Heri shaaban
Mwambawahabari
MASHINDANO ya Shule za sekondari zinazomilikiwa na Jeshi yazinduliwa mkoani Dar es Salaam.
Mashindano hayo ya mpira miguu yameshirikisha timu zote za jeshi hapa nchini kwa lengo la kuendeleza vipaji na kujenga mahusiano.
Akizungumza katika ufunguzi mashindano hayo Mwenyekiti wa Shule zinazomilikiwa na Jeshi,Kanali Robart Kessy alisema michezo hiyo itafanyika kwa mda wa wiki moja yanafanyika Katika shule yaJitegemee (
JK)sekondari.
Kanali Kessy alizitaja timu hizo Jitegemee sekondari,Kizuka,Makongo ,Kawawa,Ruhuwiko ,Kigamboni,Nyuki na Unyanyembe.
"Michezo itakayoshindanishwa katika mashindano hayo mpira miguu,wavulana,mpira pete,Netball wasichana ,mpira kikapu,Wavulana riadha,wavulana na wasichana"alisema Kessy.
Alisema michezo mingine handball,mpira miguu wasichana na wavu .
Aidha alisema michezo mingine aikushindanishwa kwa sababu mbalimbali zikiwemo uhaba wa fedha viwanja na uwanja.
Alisema hata hivyo jitihada bado zinaendelea ili kufikia lengo la kushindanisha michezo yote katika mashindanano hayo.
Akizungumzia dhumuni ĺa mashindano hayo alisema kikubwa kuendeleza vipaji kwa wanafunzi pia kujenga mahusiano sambamba kupata nafasi kwa wakuu,wa shule kutatua changamoto za elimu katika sekta ya michezo kwa ujumla.
Alitoa rai kwa jeshi liendelee kuwaunga mkono katika jitihada za kukuza vipaji vya vijana ambapo pia waliomba udhamini kwa kampuni kwa ajili ya kudhamini michezo hiyo.
Hivyo makala Shule za sekondari za Jeshi zazindua michezo ya mpira miguu
yaani makala yote Shule za sekondari za Jeshi zazindua michezo ya mpira miguu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Shule za sekondari za Jeshi zazindua michezo ya mpira miguu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/shule-za-sekondari-za-jeshi-zazindua.html
0 Response to "Shule za sekondari za Jeshi zazindua michezo ya mpira miguu"
Post a Comment