title : Makonda atoa mwezi mmoja Kampuni ya ujenzi wa Nyanza
kiungo : Makonda atoa mwezi mmoja Kampuni ya ujenzi wa Nyanza
Makonda atoa mwezi mmoja Kampuni ya ujenzi wa Nyanza
Mkuu wa mkoa Dar es saaĺam Paul Makonda akizungumza na Mkurugenzi wa Manispaa ya,Temeke Lusubilo,Mwakabibi katika ziara wilayani Temeke (Picha na Heri Shaaban)
Na Heri Shaaban
Mwambawahabari
MKUU wa Dar es Salaam Paul Makonda ametoa mwezi mmoja kwa kampuni ya Ujenzi ya Nyanza kukamilisha miradi ya ujenzi ya DMDP iliyopo wilayani Temeke ikishindwa kutekeleza agizo hilo asipewe tenda Mkoa Dar es Saĺaam.
Makonda alitoa tamko hilo Dar es Saalam leo wakati wa kukagua miradi hiyo katika ziara yake wilayani humo
"Nakuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Lusubilo Mwakabibi mfatilie huyu Mkandarasi wa Nyanza ndani ya mwezi mmoja wawe wamekamilisha ujenzi wa barabara tulizomkabidhi akishindwa atakuwa amevunja Mkataba na kukosa sifa katika mkoa huu " alisema Makonda.
Makonda alisema kampuni hiyo ilipewa mkataba wa miezi 15 kutika ujenzi wa miradi ya DMDP katika wilaya hiyo mpaka sasa miezi 11.imepita kampuni hiyo aionyeshi matumaini.
Alisema miradi hiyo ya serikali inatakiwa itekelezwe kwa wakati, ni fedha ya msaada.
Aidha alisema katika mkoa huo atafatilia kampuni zote za ujenzi akitaka ziwajibike sio kufanya kazi kwa kubabaisha.
Makonda alikagua barabara za
DMDP za Changombe km 1.9 barabara ya mchicha km 1.8 na Temeke Mbagala km 3 .5
Pia ameagiza Kampuni hiyo kujenga mitalo upya ya kuanzia eneo la Mchicha hadi Temeke Magorofani kufuatia kujenga chini ya kiwango.
Ametaka wananchi wa Temeke kutumia mifereji hiyo kwa maji ya mvua sio maji taka
Wakati huohuo Makonda amesema mara baada ya kumaliza kampeni ya usafi itafuata kampeni ya kukagua vyoo vya wananchi wa mkoa huo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Temeke
Lusubilo Mwakabibi alisema amekuja Temeke kufanya kazi atakikisha anasimamia miradi yote ya serikali kuakikisha kampuni zilizopewa tenda zinajenga kwa wakati.
Mwakabibi alisema Temeke manispaa hiyo hawakubali kuwa na wakandarasi wazembe ambao hawawajibiki.
Amewataka wakandarasi wengine katika wilaya hiyo ambao wanaomba tenda kufanya kazi kwa weledi na sio kukwamisha miradi ya serikali.
Hivyo makala Makonda atoa mwezi mmoja Kampuni ya ujenzi wa Nyanza
yaani makala yote Makonda atoa mwezi mmoja Kampuni ya ujenzi wa Nyanza Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Makonda atoa mwezi mmoja Kampuni ya ujenzi wa Nyanza mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/makonda-atoa-mwezi-mmoja-kampuni-ya.html
0 Response to "Makonda atoa mwezi mmoja Kampuni ya ujenzi wa Nyanza"
Post a Comment