title : SERIKALI YAWATAKA WANAOZUNGUKA HIFADHI YA MSITU WA KAZIMZUMBWI KUHESHIMU MIPAKA
kiungo : SERIKALI YAWATAKA WANAOZUNGUKA HIFADHI YA MSITU WA KAZIMZUMBWI KUHESHIMU MIPAKA
SERIKALI YAWATAKA WANAOZUNGUKA HIFADHI YA MSITU WA KAZIMZUMBWI KUHESHIMU MIPAKA
Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Wiliam Lukuvi akizungumza kwenye mkutano na wananchi hao katika eneo la Zingiziwa wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam. Wananchi katika eneo la Zingiziwa wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam wakimsikiliza Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Wiliam Lukuvi
*Yawazungumzia pia waliofungua kesi na baadae wakashindwa
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
SERIKALI imewataka wananchi wanaoishi kuzunguka Hifadhi ya Msitu wa Kazimzumbwi waliokuwa wamefungua kesi na baadaye kushindwa waendelee kuheshimu mipaka ya Msitu huo huku Chama Cha Mapinduzi(CCM) kikiangangalia namna bora ya kuwasaidia.
Hatua hiyo inakuja kutokana na wananchi waliokuwa na mgogoro wa ardhi ndani ya msitu kufungua kesi mwaka 2017, kwenye Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi na maamuzi ya shauri la madai ya ardhi kwenye msitu huo yaliipa serikali ushindi, baada ya wananchi hao kushindwa kuonyesha ushahidi wa umiliki wa ardhi ikiwa ni ushahidi wa manunuzi na urithi wa ardhi hiyo katika Msitu wa Hifadhi ya Kazimzumbwi,
Akizungumza kwenye mkutano na wananchi hao katika eneo la Zingiziwa wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam, Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Wiliam Lukuvi amewaambia wananchi hao kuwa hawana haki kwenye ardhi hiyo kwa mujibu wa hukumu iliyotoka,
Aliongeza kuwa mipaka ya msitu huo ipo sahihi na si vinginevyo hali iliyopelekea wananchi hao kushindwa kukata rufaa.
Hata hivyo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amejipa siku 30 kuangalia namna ya kuwasaidia wakazi wa Zingiziwa waliokuwa wamevamia msitu huo
Ameongeza kuwa tayari ameshaunda kamati iliyopewa muda wa miezi miwili kutoa na tayari ishamaliza mwezi mmoja na hivyo itatoa majibu ndani ya siku 30 lengo likiwa ni kuwasaidia wananchi hao ambao kisheria walishindwa kesi.
"Mgogoro huu ulishafika mahakamani na uamuzi ukatolewa kuwa mmevamia hilo lipo wazi na sisi hatupingani na uamuzi wa mahakama.
"Ila kwa kuwa nyie ni wananchi wetu, CCM imeamua kununua kesi, sio kwa maana ya kupinga mahakama Bali ni kwa kuangalia tunawasaidia vipi,"
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga amesema wizara yake haina tatizo na wakazi hao zaidi ya kuhakikisha msitu huo uko salama.
Amesema katika kipindi ambacho msitu huo ulivamiwa athari kubwa zilijitokeza.
"Msitu huu tunaweza kusema ndio mapafu ya Dar, sasa ukivamiwa kwa kuwekwa Makazi au shughuli za kibinadamu mambo yanakuwa mabaya,”
"Tunategemea tupate hewa nzuri kutokana huku lakini wao walivamia na kutengeneza hewa chafu. Sisi tunachosimamia ni kuhakikisha msitu unatunzwa na kubaki kuwa msitu,"amesema.
Baadhi ya wawakilishi wa kundi hilo la wananchi waliokuwa wamevamia msitu huo wameeleza kuwa wanachotaka ni kuonyeshwa mipaka ya kitaalam ya unapoanzia msitu huo.
"Hatupingani na mahakama wala wizara sisi tunataka wataalam wa wizara ya ardhi waje wafanye vipimo na kutuonyesha kitaalam ilipo mipaka," amesema Jackson Rwehumbiza.
Kuhusu msitu huo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo alisema, mwaka 1954 Serikali ilianzisha Msitu wa Hifadhi wa Kazimzumbwi wenye ukubwa wa hekta 4,860, kwa Tangazo la Serikali Na. 306 la mwaka 1954 na ramani Jb 196 ya mwaka 1954 kwa kutambua umuhimu wake.
Profesa Silayo anasema licha ya umuhimu wake Msitu wa Hifadhi wa Kazimzumbwi umekuwa ukivamiwa mara kwa mara na wananchi wanaoishi kuzunguka msitu huo na serikali ilifanya zoezi la kuwaondoa mwaka 1998,2003,3007,2011 na 2014.
“Msitu huu upo katika Wilaya ya Kisarawe na upande wa mashariki ndiyo mpaka kati ya wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani na wilaya ya Ilala mkoa wa Dar es Salaam.
Hivyo makala SERIKALI YAWATAKA WANAOZUNGUKA HIFADHI YA MSITU WA KAZIMZUMBWI KUHESHIMU MIPAKA
yaani makala yote SERIKALI YAWATAKA WANAOZUNGUKA HIFADHI YA MSITU WA KAZIMZUMBWI KUHESHIMU MIPAKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAWATAKA WANAOZUNGUKA HIFADHI YA MSITU WA KAZIMZUMBWI KUHESHIMU MIPAKA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/serikali-yawataka-wanaozunguka-hifadhi.html
0 Response to "SERIKALI YAWATAKA WANAOZUNGUKA HIFADHI YA MSITU WA KAZIMZUMBWI KUHESHIMU MIPAKA"
Post a Comment