title : SERIKALI YALETA PROGRAM YA TEKNOLOGIA YA UBUNIFU KUONGEZA WIGO WA AJIRA
kiungo : SERIKALI YALETA PROGRAM YA TEKNOLOGIA YA UBUNIFU KUONGEZA WIGO WA AJIRA
SERIKALI YALETA PROGRAM YA TEKNOLOGIA YA UBUNIFU KUONGEZA WIGO WA AJIRA
Serikali kwa kushirikiana na nchi ya Afrika ya Kusini imeanzisha programu ya Teknologia ya ubunifu katika sekta ya Afya na kilimo jambo ambalo litasaidia kutoa ajira kwa vijana na kuleta maendelea kwa Taifa.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salamm na Mtafiti Mwandamizi Idara ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt Rodgers Msuya.
Dkt. Msuya amesema kuwa program hiyo itasaidia kuleta tija baina ya nchi hizo.
Amesema kuwa katika mahusiano hayo ya teknologia ya ubunifu katika nyanja ya Afya na Kilimo yanakua na tija katika maendeleo ya nchi ikiwa ni pamoja na kutoa ajira kwa vijana.
"program hii inahusisha zaidi vijana katika kuendeleza mawazo yao ya kibunifu tunatarajia kupata ajira zaidi na pia mashirikiano kati ya nchi na nchi" amesema Dkt Msuya.
Dkt. Msuya ameongeza kuwa katika sekta hizo mbili changamo zipo, huku akitoa mfano kwa upande wa Afya amesema kuna madoa mengi yanayogundulika na mengine hayagunduliki mahali popote na mengine yanakua yakitunzwa.
” lakini kuna vijana wengine wana mawazo mazuri sana katika ugunduzi mbalimbali utakaoweza kuleta tija kwa nchi” ameongeza Dkt Msuya.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Tume ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu Dkt Amos Nungu amesema programu hiyo imewalenga zaidi vijana, watafanyakazi kwa pamoja kwa kubadilishana uzoefu katika sekta ya Kilimo na Afya ili kuweza kukabiliana na changamoto zilizopo katika sekta hizo.
” lakini tukubaliane kuwa Afrika ya Kusini wametushinda hatuko nao kiwango kimoja kiuchumi hata kisayansi na teknolojia hivyo mashirikiano yataendelea kukuza eneo letu tulilobobea tutatumia Ubunifu kutatua changamoto “amesema Dkt Nungu.
Hata hiyo Dkt Nungu ameongeza kuwa baada ya apo wataitisha watafiti na wabunifu ili waweze kushindana kati ya Afrika ya Kusini na Tanzania watashirikiana kutatua moja ya changamoto ili mbinu waliyoitumia iweze kufanyakazi Tanzania na Afrika ya Kusini, huku akisema wanaweza kushirikiana kufanya kazi kati ya mbunifu na mtafiti kwa pamoja kwani programu hii imelenga pia wabunifu.
Nae mwakilishi Balozi Afrika ya Kusini Frans Van Aarda amesema nchi yao imesaidia programu hiyo ambayo itasaidia kuendeleza ushirikiano kati ya nchi hizo katika sekta ya Afya na Kilimo pamoja na kusaidia vijana kupata ajira.
Semina hiyo imewakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo watafiti, wabunifu walioko katika sekta ya Afya,na Kilimo ili kubadilishana uzoefu katika nyanja ya sayansi na teknolojia na ubunifu ili kuona namna ya kutatua changamoto katika sekta ya Afya na Kilimo ,Semina ya siku mbili imeanza leo septemba 6 na inatarajiwa kumalizika kesho.
Hivyo makala SERIKALI YALETA PROGRAM YA TEKNOLOGIA YA UBUNIFU KUONGEZA WIGO WA AJIRA
yaani makala yote SERIKALI YALETA PROGRAM YA TEKNOLOGIA YA UBUNIFU KUONGEZA WIGO WA AJIRA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YALETA PROGRAM YA TEKNOLOGIA YA UBUNIFU KUONGEZA WIGO WA AJIRA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/serikali-yaleta-program-ya-teknologia.html
0 Response to "SERIKALI YALETA PROGRAM YA TEKNOLOGIA YA UBUNIFU KUONGEZA WIGO WA AJIRA"
Post a Comment