title : POLISI DAR YAWAONYA WATAKAOFANYA VURUGU WAKATI WA UCHAGUZI JIMBO LA UKONGA
kiungo : POLISI DAR YAWAONYA WATAKAOFANYA VURUGU WAKATI WA UCHAGUZI JIMBO LA UKONGA
POLISI DAR YAWAONYA WATAKAOFANYA VURUGU WAKATI WA UCHAGUZI JIMBO LA UKONGA
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa akionesha bastola zilizokamatwa na jeshi la polisi katika msako wa wa kutafuta waharifu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Bastola na Magazini na Risasi zilizokamatwa katika msako wa waharifu Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na msako wa waharifu jijini Dar es Salaam.
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetangaza kuimarisha ulinzi uchaguzi mdogo katika Jimbo la Ukonga na Kata ya Vingunguti unaotarajia kufanyika Septemba 16 mwaka huu.
Limesema halitamvumilia mtu yoyote atakayebainika kufanya kuvuruga katika mchakato huo na kwamba atakeyakamatwa matokeo ya uchaguzi atayasikia akiwa mikononi mwa Polisi.
Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa wakati anazungumza namna walivyoimarisha ulinzi katika maeneo ambayo uchaguzi mdogo.
Amesisitiza jeshi hilo limejipanga kuhakikisha kunakuwa na ulinzi wa kutosha kabla, baada ya uchaguzi hadi matokeo yanapotangaza na mshindi kutangazwa.
“Napenda kuwatoa hofu wananchi jeshi la Polisi limejiandaa kwa kuimarisha ulinzi na usalama wakati wa uchaguzi huo.
“Tunawaonya waliopanga kufanya vurugu watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria. Rai ya jeshi la Polisi kwa wananchi ni kutekeleza haki yao ya kikatiba kwa kufuata sheria na taratibu watakazoelekezwa siku ya hiyo na wahusika wa uchaguzi bila kuleta vurugu au wao kuwa chanzo cha vurugu,”amesema.
Mambosasa ameongeza kila kituo cha kupiga kura kutakuwa na askari wa vikosi mbalimbali kwa ajili ya kufanya doria kila sehemu wakiongozwa na askari maalumu wa kikosi cha kutuliza ghasia.
Amewahakikisha jeshi hilo kuchukua hatua za haraka za kisheria kwa mtu yeyote au kikundi chchote chenye nia ya kufanya vitendo vyovyote ambavyo ni kinyume na kanuni au sheria ya uchaguzi.
Hivyo makala POLISI DAR YAWAONYA WATAKAOFANYA VURUGU WAKATI WA UCHAGUZI JIMBO LA UKONGA
yaani makala yote POLISI DAR YAWAONYA WATAKAOFANYA VURUGU WAKATI WA UCHAGUZI JIMBO LA UKONGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala POLISI DAR YAWAONYA WATAKAOFANYA VURUGU WAKATI WA UCHAGUZI JIMBO LA UKONGA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/polisi-dar-yawaonya-watakaofanya-vurugu.html
0 Response to "POLISI DAR YAWAONYA WATAKAOFANYA VURUGU WAKATI WA UCHAGUZI JIMBO LA UKONGA"
Post a Comment