title : DKT. KIJAJI: UWEKEZAJI WA MSHAHARA NI JUKUMU LA MFANYAKAZI
kiungo : DKT. KIJAJI: UWEKEZAJI WA MSHAHARA NI JUKUMU LA MFANYAKAZI
DKT. KIJAJI: UWEKEZAJI WA MSHAHARA NI JUKUMU LA MFANYAKAZI
Na. WFM
Serikali imeeleza kuwa
uwekezaji wa mishahara kwa
wafanyakazi nchini ni
jukumu la mfanyakazi
mwenyewe kwa
kuwa mshahara ni mali ya
mfanyakazi hivyo anaweza
kuutumia kwa kuwekeza au
kuto kuwekeza.
Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa
akijibu maswali ya Mbunge wa Viti maalum Mhe. Mwantum
Dau Haji, aliyetaka kujua Serikali inasema nini kuhusu
uwekezaji wa mishahara kwa watumishi wa umma na
kuwepo kwa ucheleweshaji wa mishahara kwa Watumishi wa
Umma..
Dkt. Kijaji alieleza kuwa Serikali kwa upande wake inawalipa
mishahara wafanyakazi wake kwa wakati kwa kuzingatia
waraka wa Hazina namba 12 wa mwaka 2004 ambao
unaitaka Serikali kulipa mishahara kabla ya tarehe 25 ya kila
mwezi.
“Kumbukumbu za malipo ya mishahara kwa watumishi wa
umma zinaonesha kuwa, kuanzia Julai 2017 hadi Agosti
2018, watumishi walilipwa mishahara yao kati ya tarehe 20
na 24 ya kila mwezi hivyo napenda kuliarifu Bunge lako
Tukufu na umma kwa ujumla kuwa hakuna ucheleweshaji wa
malipo ya mishahara kwa watumishi wa umma” alieleza Dkt.
Kijaji.
Aidha Serikali imekuwa ikiwatendea haki wafanyakazi wake
katika upandishaji wa madaraja na kila mwaka wafanyakazi
hupandishwa madaraja.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango.
Hivyo makala DKT. KIJAJI: UWEKEZAJI WA MSHAHARA NI JUKUMU LA MFANYAKAZI
yaani makala yote DKT. KIJAJI: UWEKEZAJI WA MSHAHARA NI JUKUMU LA MFANYAKAZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DKT. KIJAJI: UWEKEZAJI WA MSHAHARA NI JUKUMU LA MFANYAKAZI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/dkt-kijaji-uwekezaji-wa-mshahara-ni_14.html
0 Response to "DKT. KIJAJI: UWEKEZAJI WA MSHAHARA NI JUKUMU LA MFANYAKAZI"
Post a Comment