title : NI MSIBA WA KITAIFA, VILIO VYATAWALA WAKATI WA MAZIKO YA WATU WALIOPOTEZA MAISHA
kiungo : NI MSIBA WA KITAIFA, VILIO VYATAWALA WAKATI WA MAZIKO YA WATU WALIOPOTEZA MAISHA
NI MSIBA WA KITAIFA, VILIO VYATAWALA WAKATI WA MAZIKO YA WATU WALIOPOTEZA MAISHA
*Serikali yaamua kutoa Sh.500,000 kwa kila mfiwa kusaidia mazishi, Waziri Mkuu aongoza maziko ya pamoja
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
NYUSO za majonzi,simanzi na huzuni ndizo zimetawala wakati wa mazishi ya pamoja ya makaburi ya watu tisa kati ya miili 224 ambayo imepatikana baada ya kivuko cha MV.Nyerere kupinduka.
Wakati wa maziko hayo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameongoza Watanzania katika mazishi hayo ambapo pamoja na kutoa pole amesema hatua zaidi zitaendelea kuchukuliwa kwa maofisa na watendaji ambao kwa namna moja au nyingine ni chanzo cha kutokea kwa tukio la kuzama kwa kivuko hicho.
Amesema tayari baadhi ya maofisa wanaohusika na kivuko hicho wamekamatwa na kwamba uchunguzi utaanza mara baada kuundwa kwa chombo cha kuchunguza huku akieleza majina ya watu ambao wamefariki majina yao yatandikwa sehemu moja.Akizungumza kabla ya kupuumzisha miili hiyo leo katika eneo la Ukara wilayani Ukerewe mkoani Mwanza ,Waziri Mkuu amesema ni msiba mzito na uliojaa majonzi kwa Taifa.
Amesema ni tukio la kusikitisha hasa kutokana na idadi ya watu waliofariki ambayo ni kubwa huku akielezea namna ambavyo Serikali imejipanga kuhakikisha kinapatikana kivuko cha muda ambacho kitatoa huduma ya kusafirisha abiria.Pia amesema pamoja tukio hilo ,Waziri Mkuu amesema kuna funzo ambalo wamelipata kutokana na tukio hilo na kwamba hatua mbalimbali zitachukuliwa.
Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa Rais Dk.John Magufuli ametangaza siku nne za maombelezo kuanzia Septemba 21 mwaka huu ambapo amesema bendera ya Taifa itapepea nusu mlingoti.Waziri Mkuu amesema pamoja na hatua nyingine zikiendelea kuchukuliwa yeye hataondoka eneo hilo kwani anataka kuendelea kushuhudia namna ambavyo shughuli nyingine zinaendelea na atashiriki katika kupumzisha miili.
Pia amesema Serikali imeamia kutoa Sh.500,000 kwa wafiwa kwa ajili ya kusaidia katika shughuli za kupumzisha miili ya wapendwa wao ambao wamepoteza maisha kutokana na ajali ya kupinduka kwa kivuko hocho.Wakati wa mazishi hayo viongozi mbalimbali wamepata nafasi ya kuweka mashada ya maua ambapo Waziri Mkuu alikuwa wa kwanza kuweka shada la maua katika moja ya kaburi kati ya makaburi tisa

Baadhi ya Masanduku yenye miili ya Marehemu waliofariki kufuatia kivuko cha MV Nyerere kupinduka na kuzama
Hivyo makala NI MSIBA WA KITAIFA, VILIO VYATAWALA WAKATI WA MAZIKO YA WATU WALIOPOTEZA MAISHA
yaani makala yote NI MSIBA WA KITAIFA, VILIO VYATAWALA WAKATI WA MAZIKO YA WATU WALIOPOTEZA MAISHA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NI MSIBA WA KITAIFA, VILIO VYATAWALA WAKATI WA MAZIKO YA WATU WALIOPOTEZA MAISHA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/ni-msiba-wa-kitaifa-vilio-vyatawala.html
0 Response to "NI MSIBA WA KITAIFA, VILIO VYATAWALA WAKATI WA MAZIKO YA WATU WALIOPOTEZA MAISHA"
Post a Comment