NHIF Arusha yatembea minadani kusaka wanachama

NHIF Arusha yatembea minadani kusaka wanachama - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NHIF Arusha yatembea minadani kusaka wanachama, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NHIF Arusha yatembea minadani kusaka wanachama
kiungo : NHIF Arusha yatembea minadani kusaka wanachama

soma pia


NHIF Arusha yatembea minadani kusaka wanachama

Na Seif Mangwangi, Arusha

MFUKO wa bima ya afya (NHIF), mkoa wa Arusha umewataka wakazi wa Arusha kujitokeza kwa wingi kusajili watoto wao kwenye mpango wa bima ya afya ya Toto kadi ili kuwaondolea usumbufu wa kupata matibabu na kuwapunguzia gharama.

Akizungumza katika mji wa Loliondo Ngorongoro Mkoani Arusha, jana katika zoezi la Uhamasishaji Wananchi na Jamii kwa ujumla juu ya Usajili wa Watoto kupitia Toto Afya Kadi na Usajili wa Wajasiliamali wadogo kupitia mpango wa KIKOA, afisa masoko wa mfuko huo Miradji Kisile alisema toto kadi ni mkombozi mkubwa kwa watanzania maskini.

Alisema gharama za Toto kadi ni ndogo kiasi ambacho kila mtanzania mwenye nia ataweza kuimudu na kumwezesha mtoto mdogo kupata huduma ya afya popote nchini.

Kisile alisema watendaji wa NHIF mkoa wa Arusha umeendelea kuhamasisha wakazi w mji huo kujiunga na mfuko huo na sasa wameanzisha zoezi la kuhamasisha wakazi wa Loliondo wilayani Ngorongoro kupitia Minada na Magulio yaliyopo Loliondo.

" Katika zoezi hili la hamasa tumeshapita kwenye minada ya Digodigo, Malambo, Piyaya na Wasso ambapo wananchi wamehamasika vizuri na kuahidi kujiunga," Alisema.

Kisile alisema katika zoezi hilo lililofanyika kwa siku nne kuanzia septemba 10 hadi 14 wananchi wamepata fursa ya Kuelimishwa Juu ya huduma za NHIF na jinsi ya kujisajili na mfuko wa Watoto na Wajasiliamali Wadogo Wadogo

Alisema zoezi hilo la kuhamisha litaendelea katika wilaya zingine za mkoa wa Arusha na kuhakikisha watu wengi wanajiunga na mfuko huo kwa lengo la kupata huduma bora za afya.
Afisa Masoko wa mfuko wa bima ya Afya NHIF mkoa wa Arusha Miradji Kisile akiwa katika mnada wa digodigo wilayani Ngorongoro akihamasisha wananchi wa wilaya hiyo kujiunga na huduma za bima ya afya kupitia mpango wa Kikoa na toto afya kadi


Hivyo makala NHIF Arusha yatembea minadani kusaka wanachama

yaani makala yote NHIF Arusha yatembea minadani kusaka wanachama Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NHIF Arusha yatembea minadani kusaka wanachama mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/nhif-arusha-yatembea-minadani-kusaka.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "NHIF Arusha yatembea minadani kusaka wanachama"

Post a Comment