title : NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, MH. ABDALLAH ULEGA APOKEA BOTI MBILI ZA DORIA WILAYANI KILWA
kiungo : NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, MH. ABDALLAH ULEGA APOKEA BOTI MBILI ZA DORIA WILAYANI KILWA
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, MH. ABDALLAH ULEGA APOKEA BOTI MBILI ZA DORIA WILAYANI KILWA
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Abdallah HamisUlega amekabidhi boti mbili za doria kwa BMU za Kilwa Kivinje na Mafia. Zoezi hili limefanyika katika Wilaya ya Kilwa eneo is Kivinje. Boti hizo zina thamani ya fedha za Kitanzania milioni 144 ambazo zimefadhiliwa na Umoja wa Ulaya kupitia miradi ya WWF.
Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya Bibi Jenny amesema wanafadhili miradi ya WWF hapa Tanzania yenye jumla ya bilioni 7 za Kitanzania. Aidha, amefurahi kusikia kwa uvuvi wa mabomu umepungua sana na hii ni sababu ya juhudi za serikali na wananchi wa maeneo haya. Pia alisema wao wamenunua boti ila jukumu za kuzilinda ni la Serikali ya Wilaya husika. Naye Mkurugenzi wa WWF nchini amesema wamepata taarifa kutoka kwa wavuvi kwamba sasa samaki wanaongezeka na kupatikana kwa samaki ambao walishapotea na haya yote ni kwa sababu ya kupungua kwa asilimia kubwa uvuvi wa mabomu.
Mhe Ulega Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi amesema Umoja wa Ulaya umenunua hizi boti kuunga mkono kati kubwa inayofanywa na Mhe Rais John Pombe Magufuli ya Serikali yake ya awamu ya tano. Alisema amezunguka wilaya za Mkinga, Tanga Mjini, Muheza, Pangani na Lindi kote huko wavuvi wanakiri samaki wameongezeka kwa sasa.
Ukanda huu wa Pwani hauna viwanda vya samaki na kumuomba Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya kutafuta wawekezaji kuja kuwekeza viwanda vya samaki katika mwambao wa bahari ya Hindi, pia alimuomba kufadhili ujenzi wa soko la samaki Kilwa Kivinje. Mhe. Ulega aliwaasa umoja wa vikundi vya BMU kutunza boti hizo na kuwaagiza Wilaya kusimamia ulinzi wa boti hizo. Mwisho aliwaomba WWF kuwaangalia BMU na wavuvi wa maeneo mengine kama Mkinga, Pangani, Lindi Vijijini na Mkuranga kwani nao wana mahitaji ya boti kama hizi katika ulinzi wa rasilimali zetu za bahari.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvivu, Mh. Abdallah Hamis Ulega, akizungumza akipokea mkataba kutoka Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), Jenny Correia Nunes, baada ya kusaini makubaliano ya kupokea msaada wa boti mbili za doria zenye thamani ya Shilingi Millioni 144 zilizotolewa na EU kupitia miradi ya WWF nchini kwa Wilaya mbili ya Kilwa Kivinje na Mafia katika Viwanja wa Maalim Kilwa Kivinje mkoani Lindi Tarehe 26.7.2018

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvivu, Mh. Abdallah Hamis Ulega, akizungumza na Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), Jenny Correia Nunes, na Mkurugenzi Mkazi wa WWF Tanzania, Dkt. Amani Ngusani baada ya kuwasili katika Uwanja wa Maalim Kilwa Kivinje mkoani Lindi Tarehe 26.7.2018 kupokea msaada wa boti mbili za doria zenye thamani ya Shilingi Millioni 144 zilizotolewa na EU kupitia miradi ya WWF nchini kwa Wilaya mbili ya Kilwa Kivinje na Mafia 
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvivu, Mh. Abdallah Hamis Ulega, akiwa ameongozana na Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), Jenny Correia Nunes, na Mkurugenzi Mkazi wa WWF Tanzania, Dkt. Amani Ngusani kuelekea baharini kupokea msaada wa boti mbili za doria zenye thamani ya Shilingi Millioni 144 zilizotolewa na EU kupitia miradi ya WWF nchini. 
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvivu, Mh. Abdallah Hamis Ulega, Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), Jenny Correia Nunes, na Mkurugenzi Mkazi wa WWF Tanzania, Dkt. Amani Ngusani wakisaini makubaliano baada ya kupokea msaada wa boti mbili za doria zenye thamani ya Shilingi Millioni 144 zilizotolewa na EU kupitia miradi ya WWF nchini kwa Wilaya mbili ya Kilwa Kivinje na Mafia katika Viwanja wa Maalim Kilwa Kivinje mkoani Lindi Tarehe 26.7.2018
Hivyo makala NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, MH. ABDALLAH ULEGA APOKEA BOTI MBILI ZA DORIA WILAYANI KILWA
yaani makala yote NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, MH. ABDALLAH ULEGA APOKEA BOTI MBILI ZA DORIA WILAYANI KILWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, MH. ABDALLAH ULEGA APOKEA BOTI MBILI ZA DORIA WILAYANI KILWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/naibu-waziri-wa-mifugo-na-uvuvi-mh.html
0 Response to "NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, MH. ABDALLAH ULEGA APOKEA BOTI MBILI ZA DORIA WILAYANI KILWA"
Post a Comment