MWEZI MMOJA WA KAMPENI YA USAFI MILIONI 346 ZAPATIKANA, MAKONDA ALAANI MGAMBO KUPIGA RAIA

MWEZI MMOJA WA KAMPENI YA USAFI MILIONI 346 ZAPATIKANA, MAKONDA ALAANI MGAMBO KUPIGA RAIA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MWEZI MMOJA WA KAMPENI YA USAFI MILIONI 346 ZAPATIKANA, MAKONDA ALAANI MGAMBO KUPIGA RAIA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MWEZI MMOJA WA KAMPENI YA USAFI MILIONI 346 ZAPATIKANA, MAKONDA ALAANI MGAMBO KUPIGA RAIA
kiungo : MWEZI MMOJA WA KAMPENI YA USAFI MILIONI 346 ZAPATIKANA, MAKONDA ALAANI MGAMBO KUPIGA RAIA

soma pia


MWEZI MMOJA WA KAMPENI YA USAFI MILIONI 346 ZAPATIKANA, MAKONDA ALAANI MGAMBO KUPIGA RAIA

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ametoa taarifa ya kampeni ya usafi iliyoanza takribani mwezi mmoja uliopita katika kikao kilichohusisha wadau ya afya na mazingira.

Akizungumza katika kikao hicho Makonda amesema kuwa tangu kuanza kwa kampeni hiyo zaidi ya watu 1,0000 wamekamatwa, watu 4443 waliachiwa huru, 376 walipata dhamana na takribani watu 6577 walilipa faini iliyofikia shilingi milioni 346 na laki 6 ambapo nusu ya fedha hizo ilikuwa ni malipo kwa mgambo wanaosimamia usafi na hadi sasa watu 6 bado wapo mahakamani.

Aidha amesema kuwa yeye na wakuu wa Wilaya wamelaani kitendo cha mgambo wa kusimamia usafi kumpiga raia katika eneo la Bunju na wamefatilia na hadi sasa watuhumiwa wapo katika gereza la Segerea na amewataka mgambo hao kufanya kazi kwa kufuata na kusimamia sheria kwani hakuna sheria inayorusu kupiga raia.

Aidha amewashukuru wadau na wananchi hasa wale wanaofanya usafi bila shuruti na kuwataka Wakandarasi kufanya kazi kulingana na mikataba yao na kwa kampuni zilizodanganya katika mikataba yao wajiandae kulipa gharama hizo kwa serikali.

Sambamba na hilo Makonda amewataka wanajamii wa jiji la Dar es salaam kushiriki katika shughuli za usafi na kila mmoja wa nafasi yake ashiriki suala hilo na wao kama serikali ni wasimamizi na wawezeshaji na amewataka wafanyabiashara na wenye viwanda kuweka mazingira yao katika hali ya usafi.

Pia Mkuu wa Mkoa ameeleza changamoto za mchakato huo ni pamoja na uchache wa watendaji na uchache wa mashine za EFD na ameeleza kuwa zoezi hilo ni endelevu katika kuhakikisha jiji linakuwa safi.

Naye Katibu tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Abubakar Kunenge amesema kuwa suala la usafi ni wajibu wa kila mmoja na hakuna chaguo zaidi ya kuhakikisha jiji linakuwa safi na usafi ufanyike bila shuruti na uwe tabia ya kila mmoja na amewaomba wadau wa afya na mazingira kuhamasisha katika suala zima la mazingira.

Mkutano huo umeshirikisha wadau na taasisi mbalimbali za mazingira na kujadili namna ya kuweka jiji katika hali bora zaidi.
Mkuu wa mkoa wa Dar es SalaamPaul Makonda akizungumza leo na wadau mbalimbali wa usafi katika ukumbi wa Anatoglo.(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)

 Sehemu ya wadau mbalimbali wa usafi wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (hayupo pichani)


Hivyo makala MWEZI MMOJA WA KAMPENI YA USAFI MILIONI 346 ZAPATIKANA, MAKONDA ALAANI MGAMBO KUPIGA RAIA

yaani makala yote MWEZI MMOJA WA KAMPENI YA USAFI MILIONI 346 ZAPATIKANA, MAKONDA ALAANI MGAMBO KUPIGA RAIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MWEZI MMOJA WA KAMPENI YA USAFI MILIONI 346 ZAPATIKANA, MAKONDA ALAANI MGAMBO KUPIGA RAIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/mwezi-mmoja-wa-kampeni-ya-usafi-milioni.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MWEZI MMOJA WA KAMPENI YA USAFI MILIONI 346 ZAPATIKANA, MAKONDA ALAANI MGAMBO KUPIGA RAIA"

Post a Comment