MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA AMBULANCE MALI YA JWTZ KUPATA AJALI - RPC WANKYO

MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA AMBULANCE MALI YA JWTZ KUPATA AJALI - RPC WANKYO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA AMBULANCE MALI YA JWTZ KUPATA AJALI - RPC WANKYO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA AMBULANCE MALI YA JWTZ KUPATA AJALI - RPC WANKYO
kiungo : MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA AMBULANCE MALI YA JWTZ KUPATA AJALI - RPC WANKYO

soma pia


MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA AMBULANCE MALI YA JWTZ KUPATA AJALI - RPC WANKYO

Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani (ACP) Wankyo Nyigesa akitolea ufafanuzi tukio la ajali iliyohusisha gari la kubebea wagonjwa(ambulance), Mali ya JWTZ na gari aina ya Toyota canter yenye namba za usajili T.764 ACK ,huko eneo la Kibiki, Bwilingu Chalinze Mkoani Pwani.(picha na Mwamvua Mwinyi).

NA MWAMVUA MWINYI, PWANI

ELINIKUNDA Mushi (50), amefariki dunia baada ya gari la kubebea wagonjwa (ambulance) mali ya jeshi la wananchi wa Tanzania  (JWTZ) , lililokuwa likimuwahisha hospital ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu kupata ajali eneo la Kibiki, kata ya Bwilingu, Chalinze mkoani Pwani. Katika ajali hiyo watu wengine wanne walijeruhiwa baada ya dereva wa ambulance kudaiwa kuligonga gari nyingine kwa nyuma, lililokuwa limeegeshwa pembezoni mwa barabara kwa ajili ya matengenezo .

Akitoa taarifa kuhusu tukio hilo, kamanda wa polisi mkoani Pwani, (ACP) Wankyo Nyigesa ,alisema ajali hiyo imetokea alfajiri agost 31 mwaka huu. Alieleza, gari namba 3489 JW 12 aina ya Ashok Leyland inayomilikiwa na kikosi cha jeshi 911 KJ cha Ihumwa Dodoma, mali ya JWTZ, lililokuwa likitokea Dodoma kwenda Dar es salaam aliligonga gari lingine lenye namba za usajili T. 764 ACK aina ya Toyota canter na kusababisha kifo cha mtu mmoja .

Nyigesa alisema, aliyepoteza maisha ni Elinikunda ambae alikuwa mgonjwa akipelekwa katika hospital ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi. 

"Watu wanne walijeruhiwa ambao ni pamoja na Beatrice Shidodolo (56) muuguzi wa hospital ya  Dodoma, Ufo Swai (48) mkazi wa Ngerengere yeye alikuwa akimhudumia mgonjwa akiwa Dodoma "alisema Nyigesa. 

Nyigesa aliwataja majeruhi wengine kuwa ni Justine Patrick (28) ambae alikuwa dereva wa gari namba T. 764 ACK iliyokuwa imeegeshwa kwa matengenezo na Rashid Rais (35) alikuwa fundi wa gari hilo wakazi wa Chalinze. 

Uchunguzi wa awali umebaini katika ambulance hiyo ilikuwa imepakia watu wengine wanne ambao hawakuweza kupata majeraha yoyote ambao ni MT. 3480 SGT Elimasa Mushi (40) askari wa JWTZ makao makuu ya Jeshi. 

Nyigesa aliwataja wengine kuwa ni MT 95881 PTE Taulin Kaira (30) askari wa  911 KJ aliyekuwa msindikizaji wa gari hilo la wagonjwa, Eveline Stanley (25) alipewa msaada wa usafiri na mtoto wake wa miezi 11 anaitwa Nicholous Petro na dereva wa gari hilo MT. 67451 SGT Shaban Mpwate. 

Kamanda huyo alifafanua, mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospital ya Jeshi ya Lugalo na majeruhi wamepelekwa katika hospital hiyo. Dereva wa ambulance Shaban Mpwate,anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi. 

Nyigesa aliwaasa madereva wa magari ya dharura kama magari ya wagonjwa kuhakikisha wanachukua tahadhari kubwa wanapokuwa wamepewa kipaombele na watumiaji wengine wa barabara ili kuweza kuepuka ajali zembe. 


Hivyo makala MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA AMBULANCE MALI YA JWTZ KUPATA AJALI - RPC WANKYO

yaani makala yote MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA AMBULANCE MALI YA JWTZ KUPATA AJALI - RPC WANKYO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA AMBULANCE MALI YA JWTZ KUPATA AJALI - RPC WANKYO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/mtu-mmoja-afariki-dunia-baada-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA AMBULANCE MALI YA JWTZ KUPATA AJALI - RPC WANKYO"

Post a Comment