MIRADI YA AFYA KATIKA MIKOA NA HALMASHAURI UZINGATIE THAMANI YA FEDHA.

MIRADI YA AFYA KATIKA MIKOA NA HALMASHAURI UZINGATIE THAMANI YA FEDHA. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MIRADI YA AFYA KATIKA MIKOA NA HALMASHAURI UZINGATIE THAMANI YA FEDHA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MIRADI YA AFYA KATIKA MIKOA NA HALMASHAURI UZINGATIE THAMANI YA FEDHA.
kiungo : MIRADI YA AFYA KATIKA MIKOA NA HALMASHAURI UZINGATIE THAMANI YA FEDHA.

soma pia


MIRADI YA AFYA KATIKA MIKOA NA HALMASHAURI UZINGATIE THAMANI YA FEDHA.



Na Ismail Ngayonga
MAELEZO
DAR ES SALAAM

SERIKALI imeendelea kutoa kipaumbele katika huduma za afya zenye ubora na zinazowafikia wananchi wote ili kuboresha afya zao kwa kutambua kuwa afya bora ni raslimali muhimu kwa maendeleo.

Maendeleo ya Taifa lolote la duniani yanaletwa na wananchi wenye afya na wenye uwezo wa kuzalisha mali na Serikali imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kutoa huduma za afya kwa kuzingatia sera na miongozo iliyopo.

Kabla ya Uhuru, huduma za afya nchini zilikuwa zinatolewa zaidi kwenye maeneo ya shughuli za kiuchumi kama miji na mashamba makubwa na baada ya Serikali iliweka msukumo zaidi katika kupanua huduma za afya ili kuwafikia wananchi wengi hasa walioko vijijini.

Ili kufanikisha azma hii, Serikali iliweka mfumo wa rufaa wa huduma za afya kupitia mfumo wa zahanati, vituo vya afya, hospitali za wilaya, hospitali za mikoa, maalum, kanda na taifa zilianzishwa.

Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli inaendelea kuimarisha na kuboresha huduma katika sekta ya afya  kuanzia katika ngazi ya kijiji mpaka Hospitali ya Taifa.
Moja ya mipango ya haraka inayotarajiwa kufanikishwa kwa ufanisi mkubwa na Serikali ni pamoja na kuimarisha miundombinu na mahitaji ya watumishi wa kada za afya kuanzia ngazi ya zahanati, vituo vya afya, hospitali ya wilaya na hospitali ya rufaa ya mkoa.
Katika bajeti ya Mwaka 2018/19, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), imeliomba Bunge kuiidhinisha kiasi cha Tsh Trilioni 1,458,291,418,500 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo afya, maji, elimu, barabara n.k
Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya mwaka 2018/19, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Selemani Jafo anasema Serikali imeongeza bajeti ya dawa, vifaa, vifaa tiba, chanjo na vitendanishi kutoka Tsh. Bilioni 31 zilizotengwa Mwaka 2015/16 hadi Tsh. Bilioni 269 zilizotengwa katika Mwaka 2017/18.
Anaongeza kuwa katika ya fedha hizo, Tsh. Bilioni 98.08 zimetengwa kwa ajili ya huduma ya afya ya msingi kwenye Hospitali za Wilaya, Vituo vya Afya na Zahanati pamoja na ongezeko la upatikanaji wa dawa muhimu kufikia asilimia 92 ikilinganishwa na asilimia 81 katika kipindi kama hicho Mwaka 2016.
Aidha Waziri Jafo anasema Serikali inaendelea na ujenzi na ukarabati wa Vituo vya Afya 208 ili kuviwezesha kutoa huduma za dharura za upasuaji kwa ajili ya kuboresha huduma zote za Vituo vya Afya. Kati ya Vituo hivyo 15 ni vipya na 14 ni zahanati zilizopandishwa hadhi na vituo vitatu (3) ni maboma yasiyokamilika.
“Vituo vya Afya vilivyopo ni 696 sawa na asilimia 15.7 ya lengo la kuwa na Vituo vya Afya 4,420 ambapo kati ya hivyo, vituo 513 vinamilikiwa na Serikali na vituo 183 vinamilikiwa na Sekta Binafsi na Mashirika ya Dini” anasema Waziri Jafo.
Akifafanua zaidi Waziri Jafo anasema ujenzi wa vituo hivyo utagharimu kiasi cha Tsh. Bilioni 93.5 hadi kukamilika kwake pamoja na kutenga Tsh. Bilioni 50.2 kwa ajili ya kununulia vifaa tiba pamoja na samani ili kuviwezesha kuanza kutoa huduma.
Anaongeza kuwa Ofisi yake kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto zimeandaa mkakati wa pamoja wa kukamilisha ukarabati na ujenzi wa vituo vyote ili kuboresha huduma za Afya na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kupitia wadau wa maendeleo wa Mfuko wa Pamoja wa Afya.
Sanjari na ujenzi wa vituo vya afya, Waziri Jafo anasema katika mwaka 2017/18 Serikali iliidhinishiwa na Bunge Tukufu jumla ya Tsh. Bilioni 35.5 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa Zahanati, kipaumbele kikiwa ni kukamilisha ujenzi wa maboma yaliyoanza kujengwa kwa nguvu za wananchi.
Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo imekamilisha ujenzi wa nyumba 578 za watumishi wa afya katika vituo vya afya 268 kwenye Halmashauri 51, lengo ni kuhakikisha kila kituo cha kutolea huduma za Afya kinakuwa na nyumba angalau mbili ifikapo Mwaka 2020 ili kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi” anasema Waziri Jafo.
Waziri Jafo anasema Ofisi yake pia imeanza matumizi ya mfumo wa jazia kwa kutumia Washitiri (Prime Vendor) katika Mikoa ya Dodoma, Morogoro na Shinyanga ambao lengo ni kuhakikisha dawa zinakuwepo katika vituo vya kutolea huduma za Afya endapo zimekosekana katika Bohari Kuu ya Madawa.
Anaongeza kuwa azma ya Serikali ni kuhakikisha mfumo huu unatumika katika Mikoa yote 26 nchini.

Ili kufanikisha azma ya Serikali kufikia uchumi wa kati kupitia ujenzi wa viwanda ifikapo mwaka 2025, ni dhahiri kuwa afya ndiyo mtaji na msingi mkuu wa mafanikio hayo katika uzalishaji mali katika sekta mbalimbali za maendeleo.


Hivyo makala MIRADI YA AFYA KATIKA MIKOA NA HALMASHAURI UZINGATIE THAMANI YA FEDHA.

yaani makala yote MIRADI YA AFYA KATIKA MIKOA NA HALMASHAURI UZINGATIE THAMANI YA FEDHA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MIRADI YA AFYA KATIKA MIKOA NA HALMASHAURI UZINGATIE THAMANI YA FEDHA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/miradi-ya-afya-katika-mikoa-na.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MIRADI YA AFYA KATIKA MIKOA NA HALMASHAURI UZINGATIE THAMANI YA FEDHA."

Post a Comment