MHE. MKUCHIKA ASHUHUDIA MAFANIKIO YA WANUFAIKA WA TASAF KATA YA MUHUNGA WILAYANI KASULU

MHE. MKUCHIKA ASHUHUDIA MAFANIKIO YA WANUFAIKA WA TASAF KATA YA MUHUNGA WILAYANI KASULU - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MHE. MKUCHIKA ASHUHUDIA MAFANIKIO YA WANUFAIKA WA TASAF KATA YA MUHUNGA WILAYANI KASULU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MHE. MKUCHIKA ASHUHUDIA MAFANIKIO YA WANUFAIKA WA TASAF KATA YA MUHUNGA WILAYANI KASULU
kiungo : MHE. MKUCHIKA ASHUHUDIA MAFANIKIO YA WANUFAIKA WA TASAF KATA YA MUHUNGA WILAYANI KASULU

soma pia


MHE. MKUCHIKA ASHUHUDIA MAFANIKIO YA WANUFAIKA WA TASAF KATA YA MUHUNGA WILAYANI KASULU

Mwambawahabari
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na wananchi na wanufaika wa TASAF kata ya Muhunga wilayani Kasulu, alipowatembelea ili kujionea utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini.
...........................................................
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) ameshuhudia mafanikio ya wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini waliopo kata ya Muhunga wilayani Kasulu, ambao TASAF imewawezesha kupata mahitaji mbalimbali kwa ajili ya kuboresha maisha yao.
Mhe. Mkuchika amejionea mafanikio hayo, alipowatembelea wanufaika wa TASAF, kata ya Muhunga wilayani Kasulu kwa lengo la kujionea maendeleo ya wanufaika hao wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
Kutokana na uwezeshaji wa TASAF, wanufaika hao wameweza kufanya mambo mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba za kuishi, kupata uhakika wa milo mitatu kwa siku, kununua mbuzi wa kufuga, madaftari, sare na viatu vya watoto wa shule na kujishughulisha na biashara ndogo ndogo za uchuuzi kwa ajili ya mahitaji ya nyumbani.
Mhe. Mkuchika amewataka wanufaika hao, kuhakikisha wanazitumia vema fedha za ruzuku wanazozipata kwa kuanzisha biashara ndogo ndogo kama vile kufungua duka la mahitaji ya nyumbani ili kujiongezea kipato.
Naye, mmoja wa wanufaika wa TASAF, Bi. Monica Jackson Mavuli amesema kabla ya kunufaika na TASAF, hakuwa na uwezo kiuchumi, hivyo aliishi kwenye nyumba ya nyasi, na kuongeza kuwa, fedha za TASAF zimemuwezesha kujenga nyumba ya bati ya vyumba viwili, kusomesha watoto wake na ana uhakika wa kupata chakula cha familia yake.
Mnufaika mwingine, Bi. Nezia Ndahelewe Dabi, ameishukuru Serikali kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambapo ameweza kujenga nyumba, kununua bati na kununua matofali ya kujengea jiko.
Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini ni mkombozi wa kaya maskini zilizopo katika halmashauri zinazotekeleza mpango huo.



IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI YA RAIS (UTUMISHI)

TAREHE 27 SEPTEMBA, 2018


Hivyo makala MHE. MKUCHIKA ASHUHUDIA MAFANIKIO YA WANUFAIKA WA TASAF KATA YA MUHUNGA WILAYANI KASULU

yaani makala yote MHE. MKUCHIKA ASHUHUDIA MAFANIKIO YA WANUFAIKA WA TASAF KATA YA MUHUNGA WILAYANI KASULU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MHE. MKUCHIKA ASHUHUDIA MAFANIKIO YA WANUFAIKA WA TASAF KATA YA MUHUNGA WILAYANI KASULU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/mhe-mkuchika-ashuhudia-mafanikio-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MHE. MKUCHIKA ASHUHUDIA MAFANIKIO YA WANUFAIKA WA TASAF KATA YA MUHUNGA WILAYANI KASULU"

Post a Comment