title : Mikocheni veterans ndani ya michezo ujirani mwema nchini Rwanda
kiungo : Mikocheni veterans ndani ya michezo ujirani mwema nchini Rwanda
Mikocheni veterans ndani ya michezo ujirani mwema nchini Rwanda
Timu ya Mikocheni veterans itashiriki tamasha maalum ya ujirani mwema lililopangwa kufanyika Kigali, Rwanda kuanzia Septemba 22. Timu hiyo inatarajia kuandoka nchini Septemba 19, ikiwa na wachezaji na mashabiki 23 kwa ajili ya safari hiyo kwa mujibu wa Seneta wa timu hiyo, Yassin Ally Yassin.
Yassin alisema kuwa mechi ya kwanza itakuwa dhidi ya Karibu Sports Club ya Rwanda Septemba 24 na mechi nyingine zitafuatia.
Aliwataja wachezaji wanaondoka kuwa ni Adam Mohamed Mselem, Fumu Mahamud, Dornad Mtoka, winchande Chambuso, Ally Salim, Adnan Juma, Omary Mkuku, Jumanne Mnkumbu na Hamis Kisukari.
Wengine ni Agapiti Manday, Fikir Muhango, Belanus Komba, Eric Frederic , Ian Balegele, Timothy Kipilimba, Abdul Hamis Said, Suleima Masatu, Nassoro Abdul Mwinchui, Hassan Mbegu Mohamed, Neema Visent Msema na Witness David Mbingi.
Viongozi ambao wataambatana na timu hiyo ni Chriss Chale ambaye ni Mweka Hazina, Adam Mselem (Seneta) na Aidan Mshani ambaye ni kocha. Alisema kuwa wamejiandaa vilivyo na wanatarajia kucheza mechi kadhaa za kirafiki ili kujiandaa na tamasha hilo.
“Mpaka sasa tumejiandaa vilivyo na maandalizi ya safari yetu yanakwenda vizuri, morali ya wachezaji ipo juu na tunatarajia kupata ushindi huko Rwanda,” alisema Yassin.
Alisema kuwa mbali ya kushiriki tamasha la Rwanda, pia timu yao ina mipango ya kushiriki katika matamasha mengine ya nchi za ukanda wa Afrika Mashariki ili kujifunza mambo mbalimbali na kudumisha ushirikiano na wadau wa soka.
Hivyo makala Mikocheni veterans ndani ya michezo ujirani mwema nchini Rwanda
yaani makala yote Mikocheni veterans ndani ya michezo ujirani mwema nchini Rwanda Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mikocheni veterans ndani ya michezo ujirani mwema nchini Rwanda mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/mikocheni-veterans-ndani-ya-michezo_10.html
0 Response to "Mikocheni veterans ndani ya michezo ujirani mwema nchini Rwanda"
Post a Comment