Matumizi ya Dawa za Kulevya Nchini Imepungua Kwa Kiasi cha Asilimia 90%- Mhe Majaliwa.

Matumizi ya Dawa za Kulevya Nchini Imepungua Kwa Kiasi cha Asilimia 90%- Mhe Majaliwa. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Matumizi ya Dawa za Kulevya Nchini Imepungua Kwa Kiasi cha Asilimia 90%- Mhe Majaliwa., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Matumizi ya Dawa za Kulevya Nchini Imepungua Kwa Kiasi cha Asilimia 90%- Mhe Majaliwa.
kiungo : Matumizi ya Dawa za Kulevya Nchini Imepungua Kwa Kiasi cha Asilimia 90%- Mhe Majaliwa.

soma pia


Matumizi ya Dawa za Kulevya Nchini Imepungua Kwa Kiasi cha Asilimia 90%- Mhe Majaliwa.



Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema matumizi ya dawa za kulevya nchini yamepungua kwa asilimia 90 baada ya Serikali kufanikiwa kudhibiti biashara hiyo.

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Septemba 17, 2018) baada ya kufungua mkutano wa 28 wa wakuu wa vyombo vinavyopambana na dawa za kulevya kutoka nchi za Afrika ujulikanao kama (28th HONLEA- Afrika), jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere(JNICC), unashirikisha wajumbe zaidi ya 120 kutoka nchi 54 za Afrika unatarajiwa kutoka na maazimio ya namna ya kutokomeza biashara ya dawa za kulevya katika mataifa hizo.

Waziri Mkuu amesema lengo la mkutano huo ni kubadilishana uzoefu na kupanga mikakati ya pamoja kuhusu udhibiti na mapambano dhidi ya biashara ya dawa za kulevya katika nchi hizo.

“Ni lazima tuwe na mikakati ya pamoja ya kudhibiti uzalishaji, usambazaji na matumizi ya dawa za kulevya barani Afrika. Hata hivyo ni muhimu kudhibiti njia zote zinazotumika kusafirisha dawa za kulevya.”

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Tanzania inaendelea na mikakati ya kupambana na uzalishaji wa dawa hizo ikiwemo mirungi na bangi, ambayo inapandwa kwa kuchanganywa na mazao ya chakula.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Tanzania ni nchi ya kwanza katika bara la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kuanzisha vituo vya utoaji wa matibabu kwa waathirika wa dawa za kulevya mwaka 2011.

Amesema hadi kufikia mwishoni mwa 2017, jumla vituo sita vya kutolea matibabu vilianzishwa, ambapo zaidi ya waathirika 6,500 wa dawa za kulevya aina ya heroin walijiandikisha na kupatiwa matibabu.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema matumizi ya dawa za kulevya nchini yameathiri sekta mbalimbali ikiwemo ya afya, uchumi na jamii, uchunguzi umebainisha kuwa kati ya asimilia 20 hadi 50 ya watumiaji wanamaambuzi ya ugonjwa wa ukimwi.

Amesema ni muhimu kwa nchi zote kuunga mkono na kuimarisha mifumo ya kisheria ya kimataifa katika udhibiti wa biashara za dawa za kulevya, ambao hutegemea mikataba yote ya msingi ya Umoja wa Mataifa.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, SEPTEMBA 17, 2018.


Hivyo makala Matumizi ya Dawa za Kulevya Nchini Imepungua Kwa Kiasi cha Asilimia 90%- Mhe Majaliwa.

yaani makala yote Matumizi ya Dawa za Kulevya Nchini Imepungua Kwa Kiasi cha Asilimia 90%- Mhe Majaliwa. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Matumizi ya Dawa za Kulevya Nchini Imepungua Kwa Kiasi cha Asilimia 90%- Mhe Majaliwa. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/matumizi-ya-dawa-za-kulevya-nchini.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Matumizi ya Dawa za Kulevya Nchini Imepungua Kwa Kiasi cha Asilimia 90%- Mhe Majaliwa."

Post a Comment