MARUFUKU KAMPUNI ZA UPIMAJI ARDHI BINAFSI KUPIMA ARDHI ZA WANANCHI BILA WAKUU WA WILAYA KUJUA

MARUFUKU KAMPUNI ZA UPIMAJI ARDHI BINAFSI KUPIMA ARDHI ZA WANANCHI BILA WAKUU WA WILAYA KUJUA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MARUFUKU KAMPUNI ZA UPIMAJI ARDHI BINAFSI KUPIMA ARDHI ZA WANANCHI BILA WAKUU WA WILAYA KUJUA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MARUFUKU KAMPUNI ZA UPIMAJI ARDHI BINAFSI KUPIMA ARDHI ZA WANANCHI BILA WAKUU WA WILAYA KUJUA
kiungo : MARUFUKU KAMPUNI ZA UPIMAJI ARDHI BINAFSI KUPIMA ARDHI ZA WANANCHI BILA WAKUU WA WILAYA KUJUA

soma pia


MARUFUKU KAMPUNI ZA UPIMAJI ARDHI BINAFSI KUPIMA ARDHI ZA WANANCHI BILA WAKUU WA WILAYA KUJUA

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na wakazi wa Manispaa ya Tabora katika viwanja vya Chipukizi kabla ya kuanza kutatua igogoro ya ardhi zao jana.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Tabora Bosco Nduguru akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi(hayupo katika picha)  wakati wa  ziara ya siku moja ya kiongozi huyo ya kutatua migogoro ya ardhi mkoani humo jana.
 Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Tabora ambao wana matatizo katika ardhi wakisubiri kukutana na  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (hayupo katika picha ) ili asikilize shida zao wakati wa  ziara ya siku moja ya kutatua migogoro ya ardhi mkoani humo jana.
picha na Tiganya Vincent


NA TIGANYA VINCENT- RS TABORA
SERIKALI imepiga marufuku kampuni binafisi za upimaji ardhi  ambazo zimekuwa zikiingia makubaliano ya upimaji ardhi za wananachi bila hata uongozi wa Wilaya husika kuwa na taarifa juu ya uwepo wa zoezi hili hali ambayo imesababisha baadhi ya wananchi kuwadhulumu fedha zao.

Agizo hili lilitolewa jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi baada ya wakazi wa baadhi ya maeneo ya Manispaa ya Tabora kuilalamikia Kampuni ya Ardhi Plan kuwachangisha fedha zao bila ya kupimia ardhi yao.

Alisema kuanzia sasa nchini kote hakuna Kampuni ya aina yoyote binafsi kwenda na kuingia moja kwa moja makubaliano na wananchi ya kuwapimia maeneo yao bila hata kutoa taarifa kwa uongozi wa Wilaya husika.

Lukuvi alisema Kampuni za aina hiyo zimekuwa zikiwachangisha fedha na kugawana mapato bila hata ya kuwapimia wananchi huku uongozi wa Wilaya husika hauna hata taarifa.

Alisema haiwezekani upimaji wa ardhi za wanyonge ukageuza uchochoro wa kuwaibia na kuwadhulumu wananachi haki zao na kuongeza kuwa lazima sheria na taratibu zifuatwe katika upimaji wa ardhi za wananchi na taarifa ziwe kwa Wakuu wa Wilaya.

Aidha Waziri huyo alizitaka Halmashauri zote za Mkoa wa Tabora kutumia Chuo cha Ardhi Tabora na kuachana na Kampuni za nje kupima ardhi ili kuepuka matumizi makubwa ya gharama za zoezi hilo.

Alisema hakuna sababu ya Tabora kuendelea kuwa na maeneo ambayo yanajengwa kiholela holela wakati wanao wataalamu katika Chuo cha Ardhi ambao wameshindwa kuwatumia.

Katika hatua nyingine Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Lukuvi alizitaka Taasisi zote za Umma kuhakikisha maeneo yao wanayomiliki yamepima na wanazo hati kabla ya kumalizika kwa mwa mwaka huu.

Alisema baada ya kupima wanatakiwa kuweka alama katika mipaka ya maeneo yao ili kuepuka wananchi kuyavamia na kujenga na kusababisha migogoro ambayo inaweza kuzuilika.

Wakati huo huo Lukuvi ameuagiza Uongozi wa Manispaa ya Tabora kuhakikisha wanakamilisha uandaaji wa hati miliki za  viwanja 938 katika eneo la Malabi na kuwakabidhi wamiliki wake kabla ya kumalizika kwa mwaka huu.
Alisema hatua ya kuendelea kukaa na viwanja hivyo bila kutoa hati kwa wahusika kwa miaka mitatu iliyopita kumesababishia hasara Serikali ya kukosa kodi ya ardhi kutoka kwa wahusika.

Waziri huyo aliwataka wakazi wa Malabi kuanzia Jumatatu ijayo ambao wameshipimiwa maeneo yao kwenda kuviripia ili hatimaye wapate hati.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alikuwa katika ziara ya siku moja ya kutatua migogoro ya ardhi ambapo alifanikiwa kusikiliza migogoro ardhi zaidi ya 540 na kuipatai majibu.



Hivyo makala MARUFUKU KAMPUNI ZA UPIMAJI ARDHI BINAFSI KUPIMA ARDHI ZA WANANCHI BILA WAKUU WA WILAYA KUJUA

yaani makala yote MARUFUKU KAMPUNI ZA UPIMAJI ARDHI BINAFSI KUPIMA ARDHI ZA WANANCHI BILA WAKUU WA WILAYA KUJUA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MARUFUKU KAMPUNI ZA UPIMAJI ARDHI BINAFSI KUPIMA ARDHI ZA WANANCHI BILA WAKUU WA WILAYA KUJUA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/marufuku-kampuni-za-upimaji-ardhi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MARUFUKU KAMPUNI ZA UPIMAJI ARDHI BINAFSI KUPIMA ARDHI ZA WANANCHI BILA WAKUU WA WILAYA KUJUA"

Post a Comment