title : Kamati za Bunge Zaishauri Serikali Kutekeleza Miradi ya Maendeleo Kwa Ubia na Sekta Binafsi.
kiungo : Kamati za Bunge Zaishauri Serikali Kutekeleza Miradi ya Maendeleo Kwa Ubia na Sekta Binafsi.
Kamati za Bunge Zaishauri Serikali Kutekeleza Miradi ya Maendeleo Kwa Ubia na Sekta Binafsi.
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Miundombinu,
Bajeti na Kamati ya Uwekezaji na Mitaji, wameishauri
Serikali kutekeleza kwa vitendo miradi mikubwa na yenye tija
kwa Umma kwa kutumia njia ya Ubia kati ya Umma na Sekta
binafsi ili kuchochea haraka maendeleo ya nchi.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Bajeti Mhe. Mashimba Ndaki amesema kuwa wabunge
wameridhishwa na na hatua zinazochukuliwa na Serikali
katika kuhakikisha kuwa mpango wa ubia kati ya Serikali na
sekta binafsi unafanikiwa na unachochea maendeleo ya
wananchi.
“Kama wabunge tungependa kuona mpango unaingizwa
katika mipango ya Serikali ili kuharakisha miradi ya
maendeleo na pia tunapongeza hatua zilizochukuliwa na
Serikali ikiwemo kumteua Kamishna anayeshughulikia
miradi ya ubia kati ya sekta binafsi na ile ya umma, “
Alisisitiza Mboya
Alibainisha kuwa jukumu la Serikali ni kuhakikisha kuwa
inaweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wote
watakaojitokeza kushirikiana na Serikali katika kutekeleza
miradi ya maendeleo hapa nchini.
Mwenyekiti wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi
Mhe. Endrew Chenge amesema kuwa nchi nyingi Duniani
zimefanikiwa kuwaletea wananchi wake maendeleo kupitia
utaratibu huo ambapo jambo la muhimu ni kufanywa kwa
maandalizi ya kina na kuwepo kwa utashi kutasaidia
kufanikiwa kwa miradi husika .
Aliongeza kuwa mwaka huu Serikali imeleta Bungeni
Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya PPP utakaojadiliwa na
wabunge katika Bunge linaloanza Septemba 4 mwaka huu,
pamoja na mambno mengine Muswada huo unapendekeza
kuanzishwa kwa Kituo cha PPP chini ya Wizara ya Fedha na
Mipango, ambacho kitakuwa na jukumu la kuishauri Serikali
kuhusu masuala yanayo husu miradi mbalimbali
itakayowasilishwa kwa mfumo wa Ubia kati ya Sekta ya
Umma na Sekta Binafsi
Akizungumza katika Semina hiyo, Kamishna wa Ubia kati ya
Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Wizara ya Fedha na
Mipango, Dkt. John Mboya amesema kuwa Dhamira ya
Serikali ni kuhakikisha kuwa inaweka mazingira wezeshi
katika kutekeleza miradi ya ubia na Sekta binafsi ili kuleta
mageuzi katika maisha ya wananchi.
“Lengo la kuwa na miradi ya ubia kati ya Serikali na sekta
binafsi ni kutekelezaIilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM),
kutekeleza mpango wa maendeleo na hatimaye kutoa
huduma bora kwa wananchi,” Alisisitiza Mboya
Akifafanua Mboya amesema kuwa moja ya hatua za
maboresho zilizochukuliwa na Serikali ni kuhamisha Kituo
cha kusimamia miradi ya ubia katika ya Umma na Sekta
binafsi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kuja Wizara ya Fedha.
Akizungumzia majukumu ya chombo cha kusimamia
utekelezaji wa miradi hiyo Dkt. Mboya amesema kuwa
chombo hicho kimepewa jukumu la kufanya uchambuzi wa
kina kuhusu miradi yenye sifa na kusimamia mchakato wa
uteklezaji wa mpango huo kwa kufuata ngazi zote zilizopo
hadi utekelezaji wa mradi husika.
Aliongeza kuwa ili kufanikisha mpango huo Serikali
inasisistiza uwazi, uwajibikaji na utayari hali itakayo
sababisha kufikiwa kwa malengo ya miradi ya ubia kati ya
sekta hizo mbili ambapo alitaja baadhi ya miradi
itakayotekelezwa ambayo upembuzi yakinifu umekamilika
kuwa ni ile ya ujenzi wa Viwanda vya dawa, usambazaji wa
gesi majumbani katika Jiji la Dar es Salaam, Mtwara , Lindi
na ule wa uendeshaji wa mabasi ya mwendo kasi Jijini Dar
es Salaam ambao umeanza na uko katika hatua mbalimbali
za uendelezwaji.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya
Dawa (MSD) Bw. Laurean Bwanakunu amesema kuwa tayari
Bohari hiyo imekamilisha upembuzi yakinifu wa mradi wa
ujenzi wa viwanda vya dawa na vifaa tiba vinavyotokana na
malighafi zinazozalishwa hapa nchini ikiwemo pamba na
kufikia machi mwakani zabuni ya mradi huo itatangazwa ili
kuwapata wabia.
Katika kutekeleza mradi huo kiwanda cha kuzalisha maji ya
dripu yanayotumika kwa wagonjwa mahosipitalini pia
kitajengwa ambapo kwa sasa maji hayo yanaagizwa kutoka
nchini Uganda na kwamba hatua hiyo itapunguza gharama
za Serikali za kuagiza dawa na vifaa hivyo kutoka nje ya nchi
ambapo zaidi ya shilingi trilioni 1.8 hutumika kuagiza
bidhaa hizo kila mwaka.
Kwa upande wake. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Maendeleo ya Petroli (TPDC) Mhandisi Kapuulya Musomba
amesema kuwa mradi wa kusambaza gesi majumbani katika
Jiji la Dar es Salaam, Mtwara na Lindi unaotarajiwa
kuhgaribu zaidi ya shilingi bilioni 300, utaleta mageuzi kwa
wananchi wa mikoa hiyo ambapo wananchi zaidi ya 120,000
katika Jiji la Dar es Salaam watafikiwa.
Aliongeza kuwa katika mikoa ya Lindi na Mtwara wananchi
zaidi ya 5,000 wataunganishiwa gesi majumbani mwao huku
viwanda zaidi 30 katika maeneo ya mradi vitaunganishiwa
huduma hiyo pamoja na vituo vya kujaza gesi kwenye magari
yanayotumia nishati hiyo.
Semina kwa wabunge wa Kamati za Bajeti, Miundombinu na
ile ya Uwekezaji Mitaji imefanyika Jijini Dodoma
ikiwashirikisha wajumbe wa Kamati hizo ili kuwajengea
uwezo wa namna dhana hiyo inavyoweza kuleta maendeleo
hapa nchini.
Hivyo makala Kamati za Bunge Zaishauri Serikali Kutekeleza Miradi ya Maendeleo Kwa Ubia na Sekta Binafsi.
yaani makala yote Kamati za Bunge Zaishauri Serikali Kutekeleza Miradi ya Maendeleo Kwa Ubia na Sekta Binafsi. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Kamati za Bunge Zaishauri Serikali Kutekeleza Miradi ya Maendeleo Kwa Ubia na Sekta Binafsi. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/kamati-za-bunge-zaishauri-serikali.html
0 Response to "Kamati za Bunge Zaishauri Serikali Kutekeleza Miradi ya Maendeleo Kwa Ubia na Sekta Binafsi."
Post a Comment