Dkt. Ndugulile - Familia Zilizotelekezwa Zitoe Taarifa Ofisi za Ustawi wa Jamii

Dkt. Ndugulile - Familia Zilizotelekezwa Zitoe Taarifa Ofisi za Ustawi wa Jamii - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Dkt. Ndugulile - Familia Zilizotelekezwa Zitoe Taarifa Ofisi za Ustawi wa Jamii, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Dkt. Ndugulile - Familia Zilizotelekezwa Zitoe Taarifa Ofisi za Ustawi wa Jamii
kiungo : Dkt. Ndugulile - Familia Zilizotelekezwa Zitoe Taarifa Ofisi za Ustawi wa Jamii

soma pia


Dkt. Ndugulile - Familia Zilizotelekezwa Zitoe Taarifa Ofisi za Ustawi wa Jamii

Image result for picha ya Faustine Ndugulile
Na: Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.
Serikali imetoa wito kwa wazazi/walezi na wote wenye jukumu la kutoa malezi na matunzo kwa watoto kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kikamilifu.
Wito huo umetolewa leo, Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia  Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Amina Nassor Makilagi kuhusu mkakati wa Serikali wa kuweka sheria kali itakayowabana wazazi ambao wamekuwa wakitelekeza watoto na familia zao.
"Matunzo, malezi na ulinzi wa mtoto ni haki ya mtoto kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009. Aidha kifungu cha 7 - 9 kinatoa majukumu kwa mzazi/mlezi na mtu yeyote mwenye jukumu la kumlea mtoto kuhakikisha anawatunza na kuwalea watoto, ikiwemo kuwapatia huduna zote muhimu, kama chakula, malazi, mavazi, elimu na kuwalinda na vitendo vya unyanyasaji, ukatili, unyonyaji na utekelezaji," alisema Dkt. Ndugulile.
Ameendelea kusema kuwa kifungu cha 14 cha Sheria ya Mtoto kinatoa adhabu kwa mzazi/mlezi yeyote atakayekiuka kifungu hiki atatozwa faini isiyozidi shilingi milioni tano au kifungo kisichozidi miezi sita au vyote viwili kwa pamoja.
Vile vile amesema, kwa kipindi cha 2016/2017 jumla ya mashauri 6557 yanayohusu matunzo na malezi ya watoto na wanawake yalishughulikiwa katika ngazi ya Mamlaka za Halmashauri na Serikali za Mitaa.
Aidha, Dkt. Ngugulile amezitaka familia zilizotelekezwa kutoa taarifa kwenye ofisi za Ustawi wa Jamii zilizoko katika Halmashauri wanazoishi ili mashauri yao yaweze kusikilizwa na watoto kupata huduma stahiki kwa ajili ya makuzi yao.

Pia ametoa wito kwa Maafisa Ustawi wa Jamii katika ngazi zote za Serikali kuhakikisha wanashughulikia kwa haraka mashauri yanayowasilishwa kwenye ofisi za kwa kutumia sheria na taratibu zilizopo.


Hivyo makala Dkt. Ndugulile - Familia Zilizotelekezwa Zitoe Taarifa Ofisi za Ustawi wa Jamii

yaani makala yote Dkt. Ndugulile - Familia Zilizotelekezwa Zitoe Taarifa Ofisi za Ustawi wa Jamii Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Dkt. Ndugulile - Familia Zilizotelekezwa Zitoe Taarifa Ofisi za Ustawi wa Jamii mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/dkt-ndugulile-familia-zilizotelekezwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Dkt. Ndugulile - Familia Zilizotelekezwa Zitoe Taarifa Ofisi za Ustawi wa Jamii"

Post a Comment