title : DKT. MWAKYEMBE SOKO GEITA.
kiungo : DKT. MWAKYEMBE SOKO GEITA.
DKT. MWAKYEMBE SOKO GEITA.
Kwa upande wa soka (wakubwa), timu ya Ushirombo Renjaz (Rangers) iliibuka mshindi baada ya kuichabanga timu ya Lyamba Mgongo bao 2-0 na kujinyakulia kitita cha shilingi laki tano, jezi seti tatu, mipira mitatu pamoja na kombe.
Mshindi wa pili timu ya Lyamba Mgongo ilijinyakulia shilingi laki tatu, jezi seti mbili na mipira mitatu huku mshindi wa tatu timu ya Kazibizyo FC akijinyakulia shilingi laki mbili, jezi seti moja na mpira mmoja.
Kwa upande wa watoto, timu za Simba na Yanga zilitoshana nguvu kwa sare ya bao 1-1 na hivyo kila timu kujinyakulia shilingi 25,000 huku mfungaji bora Carol Frances na mlinda mlango bora Casto Paul wote wakiibuka na shilingi elfu hamsini kila mmoja.
Michezo mingine ilikuwa ni kuvuta kamba ambapo kwa upande wa wanaume Simba waliibuka mshindi dhidi ya Yanga na kujinyakulia shilingi elfu hamsini huku upande wa wanawake Yanga wakiibuka washindi dhidi ya Simba na kujishindia shilingi elfu hamsini pia.
Kwenye mchezo wa Karate, Shotokan walijishindia elfu hamsini, mpira wa wavu PVC walijishindia elfu hamsini, mbio za mita 100 wanaume mshindi alikuwa Projestus Rutha na wanawake ushindi ulienda kwa Tumain Mwasilembo ambapo kila mmoja alijinyakulia
shilingi elfu hamsini, mpira wa pete timu ya Kurugenzi alijinyakulia pia shilingi elfu hamsini.
Mbio za baiskeli mshindi mshindi wa kwanza Furaha Joseph alijinyakulia elfu sitini na mshindi wa pili Subi Kachila akijishindia shilingi elfu 40, mbio za magunia upande wa wanaume mshindi alikuwa Daniel Ishike na wanawake alikuwa Linda Deo ambapo
kila mmoja alijishindia shilingi elfu hamsini huku mbio za kuku wanaume na wanawake kila mshindi akiondoka na kuku.
Akizungumza kwenye fainali za mashindano hayo, Waziri Dkt. Mwakyembe alikiri suala la ubovu wa viwanja vya michezo katika halmashauri mbalimbali nchini ikiwemo Bukombe na kutoa
rai kwa halmashauri kuweka mikakati ya kuboresha viwanja hivyo na kwamba serikali itaunga mkono juhudi hizo ili kuhakikisha vinakuwa bora kwani michezo ni ajira.
Mashindano hayo yalianza Julai 27, 2018 yakiandalia na mbunge wa jimbo la Bukombe, Doto Mashaka Biteko (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini yakiwa na lengo la kuibua na kuendeleza vipaji, kuchochea maendeleo na kuimarisha umoja huku
kaulimbiu ikiwa ni “Kusema na Kutenda”
Hivyo makala DKT. MWAKYEMBE SOKO GEITA.
yaani makala yote DKT. MWAKYEMBE SOKO GEITA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DKT. MWAKYEMBE SOKO GEITA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/dkt-mwakyembe-soko-geita.html
0 Response to "DKT. MWAKYEMBE SOKO GEITA."
Post a Comment