title : DAWASA, TIC, TTCL WAMPONGEZA MHANDISI MFUGALE
kiungo : DAWASA, TIC, TTCL WAMPONGEZA MHANDISI MFUGALE
DAWASA, TIC, TTCL WAMPONGEZA MHANDISI MFUGALE
Na Mwandishi Wetu.Globu ya Jamii
VIONGOZI wa wanachama wa Jukwaa la Wakuu wa Taasisi za Serikali Tanzania waliamua kwa pamoja kumpongeza Afisa Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale kwa kutambuliwa na Serikali hususani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kwa umahiri na utumishi uliotukuka.
Akizindua flyover ya Tazara ambayo imepewa jina la Mfugale, Rais alisema anajua uzalendo, uaminifu na ubunifu wa mhandisi huyo amabaye siku zote amesimama imara na kuchapa kazi mpaka kufanikisha ujenzi wa Flyober hiyo.
Wakiwa katika kikao chao cha kawaida cha mwezi, viongozi hao wa Taasisi za umma walisema kila mwananchi anatambua mchango wa mhandisi Mfugale katika kujenga uchumi wa nchi kupitia uimarishwaji wa sekta ya usafiri wa barabara.
Viongozi hawa wa taasisi hukutana kila mwezi wakiwa na lengo la kujadili njia bora za kuharakisha maendeleo ya nchi kupitia sekta wanazoziongoza. Aidha katika vikao hivyo hubadilishana uzoefu na kujadili namna ya kupambana changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.
Mhandisi Cyprian Luhemeja akimpongeza mtendaji mkuu wa TANROADS mhandisi Partick Mfugale baada ya kufanikisha kwa ujenzi wa Flyover ya Tazara iliyozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli jana Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu Shirika la Simu TTCL Waziri Kindamba akimpa zawadi ya pongezi Mtendaji mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale baada ya kufanikisha kwa ujenzi wa Flyover ya Tazara iliyozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli jana Jijini Dar es salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Taifa cha Uwekwzaji TIC Geoffray Mwambe akimpongeza Mhandisi Mfugale baada ya kufanikisha kwa ujenzi wa Flyover ya Tazara iliyozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli jana Jijini Dar es salaam.
Picha ya pamoja.
Hivyo makala DAWASA, TIC, TTCL WAMPONGEZA MHANDISI MFUGALE
yaani makala yote DAWASA, TIC, TTCL WAMPONGEZA MHANDISI MFUGALE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DAWASA, TIC, TTCL WAMPONGEZA MHANDISI MFUGALE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/dawasa-tic-ttcl-wampongeza-mhandisi.html
0 Response to "DAWASA, TIC, TTCL WAMPONGEZA MHANDISI MFUGALE"
Post a Comment