title : WATANZANIA WAKARIBISHWA JUKWAA LA BIASHARA GEITA
kiungo : WATANZANIA WAKARIBISHWA JUKWAA LA BIASHARA GEITA
WATANZANIA WAKARIBISHWA JUKWAA LA BIASHARA GEITA
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel amewakaribisha wananchi wa mkoa huo, mikoa ya jirani na Tanzania kwa ujumla kuhudhuria katika Jukwaa la Fursa za Biashara mkoani Geita linalofanyika leo.
Kiongozi huyo amesema ana hakika litakuwa na manufaa makubwa kwa mkoa wake. Mkuu wa Mkoa amewaeleza waandishi wa habari ofisini kwake kuwa, Jukwaa hilo limetanguliwa na maonesho ya bidhaa za wajasiriamali zinazozalishwa Geita.
Amesema maonesho hayo yaliyoanza jana katika viwanja vya Halmashauri ya Mji wa Geita na kwamba yatamalizika kesho sambamba na Jukwaa la Biashara. Alisema Jukwaa litafanyikia katika ukumbi wa Gedeco unaomilikiwa na Halmashauri hiyo ya Mji wa Geita.
Gabriel amesema nia kubwa ya kufanyika kwa Jukwaa na maonesho hayo ni kuwasaidia wajasiriamali wa mkoa wake kutangaza fursa walizo nazo sambamba na kukutana na wadau mbalimbali wa maendeleo na hivyo kujifunza kutoka kwao ili kuweza kupanuka zaidi kibiashara.
"Wajasiriamali watakapokutana na wadau mbalimbali wa biashara kwenye jukwaa kesho, watakuwa wanaongea lugha moja ya biashara na uwekezaji ili kunyanyua mkoa wa Geita," alisema.
Alisema katika jukwaa hilo, ana hakika wajasiriamali wa Geita watapata ujuzi, elimu na hata masoko kwa ajili ya kuboresha shughuli zao.
"Wajasiriamali wetu watakutana na taasisi za fedha na kujua ni taasisi ipi inaweza kuwasadia kukuza mitaji yao," alisema.
Alisema jukwaa hilo pia linausaidia mkoa kutangaza fursa zake kwa Watanzania, fursa ambazo zimekuwa pia zikiandikwa na vyombo mbalimbali vya habari, hususani vya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN).
Mkuu wa mkoa ameishukuru TSN kwa kuanzisha majukwaa ya biashara na kuwa tayari kushirikiana na ofisi yake ili kufanikisha Jukwaa la Biashara la kesho.
Kaimu Mhariri Mtendaji wa TSN, Tuma Abdallah, amesema ana matarajio makubwa kwamba Jukwaa la Biashara la kesho litakuwa na msisimko wa aina yake kutokana na maandalizi yaliyofanyika na hasa ushirikiano mkubwa uliotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita.
Akielezea kwa nini TSN imeamua kufanya majukwaa ambapo hili ya Geita ni la saba, Tuma amesema ni kutokana na kuona kwamba taasisi hiyo ya serikali ina dhima ya kusaidia na kuleta chachu katika kuboresha biashara na uwekezaji kwa maendeleo ya taifa.
Amesema, lengo la majukwaa hayo ni kuibua fursa za biashara na uwekezaji katika maeneo husika.
Alisema timu ya TSN imekaa mkoani Geita kwa karibu wiki tatu, imetembea maeneo mbalimbali ya mkoa na kuzungumza na wadau mbalimbali kuhusu maendeleo ya mkoa wa Geita na kisha kusambaza habari za maeneo hayo na kwamba kesho kutakuwa na toleo maalumu la mkoa wa Geita kwenye gazeti hili.
Tayari kampuni kadhaa zimejitokeza kudhamini Jukwaa la Geita ikiwa Geita Gold Mine (GGM), Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Maelezo Televisheni, TADB Bank, Benki ya NBC na Busolwa Mining Limited.
Wadhamini wengine ni Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko Hifadhi ya Jamii (SSRA), Benki ya Azania, Lenny Hotel, Waja General Company Ltd, GF Truck, Air Tanzania Corporation Ltd, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA).
Hivyo makala WATANZANIA WAKARIBISHWA JUKWAA LA BIASHARA GEITA
yaani makala yote WATANZANIA WAKARIBISHWA JUKWAA LA BIASHARA GEITA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATANZANIA WAKARIBISHWA JUKWAA LA BIASHARA GEITA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/watanzania-wakaribishwa-jukwaa-la.html
0 Response to "WATANZANIA WAKARIBISHWA JUKWAA LA BIASHARA GEITA"
Post a Comment