title : Wataalam wa afya kutoka Japan watembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
kiungo : Wataalam wa afya kutoka Japan watembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
Wataalam wa afya kutoka Japan watembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
Wataalam wa afya kutoka nchini Japan leo wametembelea hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kufanya mazungumzo na uongozi wa Hospitali hiyo.
Katika mazungumzo yao watalaam hao wamepata fursa ya kubadilishana uzoefu wa utoaji huduma za afya na kujadiliana namna ambavyo wanaweza kushirikiana katika maeneo mbalimbali ya utoaji huduma .
Mkurugenzi wa huduma za tiba Dkt. Hedwiga Swai amesema MNH ina mipango mbalimbali ya kuboresha huduma zake za ubingwa wa juu ikiwemo upandikizaji figo na kusisitiza kuwa huduma hiyo ni endelevu na imekuwa na mafanikio makubwa tangu ilipoanzishwa kwa mara ya kwanza nchini Novemba mwaka jana .
“Lengo letu ni kuhakikisha huduma za kibingwa zinakuwa endelevu lakini pia kama hospitali mipango yetu ni kuanzisha huduma zingine mpya ambazo hapo awali hazikuwepo”amesema Dkt. Swai.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa huduma za tiba shirikishi Dkt. Praxeda Ogweyo amesema pamoja na mafanikio ambayo Muhimbili imepata lakini pia kuna changamoto ya upungufu wa watalaam katika maeneo mbalimbali ya utoaji huduma
Wakurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) pamoja na wataalam wa afya kutoka Japan wakijadiliana juu ya utoaji wa huduma bora za afya .
Mmoja wa wataalam kutoka Japan Yoshio Mikamo akielezea ambavyo huduma za afya zinatolewa nchini humo.
Wakurugenzi wa vitengo mbalimbali vya Hospitali ya Taifa Muhimbili wakisikiliza maelezo yanayotolewa na mtaalam huyo.
Mkuu wa Idara ya Famasia MNH Deus Buma akiwaelezea wataalam hao kuhusiana na huduma za utoaji dawa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili mara baada ya kutembelea moja ya maduka ya dawa ya hospitali hiyo.
Meneja wa jengo la wagonjwa wa nje Sista June Samwel akifafanua
huduma zinazotolewa katika jengo hilo
Hivyo makala Wataalam wa afya kutoka Japan watembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
yaani makala yote Wataalam wa afya kutoka Japan watembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wataalam wa afya kutoka Japan watembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/wataalam-wa-afya-kutoka-japan.html
0 Response to "Wataalam wa afya kutoka Japan watembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili"
Post a Comment