title : UVCCM Wilaya ya Ilala yawafunda vijana wake
kiungo : UVCCM Wilaya ya Ilala yawafunda vijana wake
UVCCM Wilaya ya Ilala yawafunda vijana wake
Na Heri Shaban
Mwambawahabari
UMOJA wa Vijana wa UVCCM Wilaya ya Ilala yataka vijana wake Kitunza shahada zao za kupiga kura ili wazitumie katika chaguzi Jimbo la UKONGA na udiwani katika Kata VINGUNGUTI na Zingiziwa .
Hayo yalisemwa Dar es salaam Leo na Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Ilala Hamadi Pazi wakati wa maadhimisho ya siku ya Vijana Duniani ambapo wilaya ya Ilala wameazimisha kwa kushiriki shughuli za kijamii kufanya usafi Shule ya Mnazi Mirefu na, Air Wing pamoja na Bonanza mbalimbali.
"Tumeazimisha siku ya Vijana na VIJANA wangu wa Wilaya ya Ilala katika maadhimisho Mgeni rasmi Ofisa Vijana Wilaya ya Ilala Mara baada maadhimisho hayo tulitoa elimu kwa Vijana kuwataka wajiandae kwa chaguzi ndogo za ubunge na udiwani "alisema Pazi.
Pazi alisema Wilaya ya Ilala inatarajia kuingia katika uchaguzi mdogo Septemba mwaka huu wa Ubunge Jimbo la Ukonga na baadhi ya Kata Wilayani Ilala hivyo aliwaasa vijana wake watunze shahada zao za kura wasirubuniwe waje watumie kuja kupiga kura ni haki yao ya msingi.
Pazi aliwataka vijana wa wilaya ya Ilala kuchagua CCM ndio inatekeleza ILANI katika Serikali iliyo madarakani hivyo wasirubunike kuuza shahada kupiga kura ni haki ya kila mtu.
Kwa upande wake KATIBU wa UVCCM wilaya ya Ilala Irene Molle alisema aliwaasa Vijana wake kusimamia misingi ya chama na kanuni ya Vijana.
Irene aliwataka vijana wa Wilaya ya Ilala kufanya kazi za jumuiya hiyo kwa weledi bila kuyumbishwa na kujenga mahusiano na jamii.
"Maudhui ya siku hii kutoa elimu ya mikopo ya ujasiriamali kwa Vijana, Pia vijana nguzo katika TAIFA na ushiriki wa Vijana katika kuijenga Tanzania MPYA alisema " Irene
Naye Katibu wa Hamasa na Chipukizi Wilaya hiyo, Fadiga Legele alisema kwa sasa vijana ni wakati wetu kuamka na kuchangamkia fursa Rais wa awamu ya tano ameonyesha kutuamini na sisi tunaaidi atutamuangusha katika kutekekeza majukumu yetu.
Hivyo makala UVCCM Wilaya ya Ilala yawafunda vijana wake
yaani makala yote UVCCM Wilaya ya Ilala yawafunda vijana wake Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UVCCM Wilaya ya Ilala yawafunda vijana wake mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/uvccm-wilaya-ya-ilala-yawafunda-vijana.html
0 Response to "UVCCM Wilaya ya Ilala yawafunda vijana wake"
Post a Comment