UPANDE WA MASHTAKA WAPEWA SIKU SABA KUKAMILISHA MCHAKATO KUBADILI HATI YA MASHTAKA KESI YA AKINA AVEVA, NYANGE

UPANDE WA MASHTAKA WAPEWA SIKU SABA KUKAMILISHA MCHAKATO KUBADILI HATI YA MASHTAKA KESI YA AKINA AVEVA, NYANGE - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UPANDE WA MASHTAKA WAPEWA SIKU SABA KUKAMILISHA MCHAKATO KUBADILI HATI YA MASHTAKA KESI YA AKINA AVEVA, NYANGE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UPANDE WA MASHTAKA WAPEWA SIKU SABA KUKAMILISHA MCHAKATO KUBADILI HATI YA MASHTAKA KESI YA AKINA AVEVA, NYANGE
kiungo : UPANDE WA MASHTAKA WAPEWA SIKU SABA KUKAMILISHA MCHAKATO KUBADILI HATI YA MASHTAKA KESI YA AKINA AVEVA, NYANGE

soma pia


UPANDE WA MASHTAKA WAPEWA SIKU SABA KUKAMILISHA MCHAKATO KUBADILI HATI YA MASHTAKA KESI YA AKINA AVEVA, NYANGE

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa siku saba kwa upande wa mashtaka kukamilisha mchakato wa kubadilisha hati ya mashtaka kwa kuwaondoa Zacharia Hans Poppe na Franklin Lauwo ili kesi dhidi ya washtakiwa Evans Aveva na Godfrey Nyange iweze kuendelea.

Amri hiyo, imetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba baada ya Wakili wa Takukuru, Leonard Swai kueleza mahakamani hapo kesi imepangwa kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa Aveva na Nyange wapo mahakamani.

Amedai mara ya mwisho Mahakama ilitoa agizo la kuwaondoa Poppe na Lauwo katika hati ya mashtaka ili kesi iendelee kwa Aveva na Nyange.
Amedai utaratibu umefanyika na jalada limepelekwa kwa DPP na amejitahidi kulifuatilia hadi leo asubuhi na ametoka kwa DPP lakini hajaweza kulishughulikia, yupo nje ya Dar es Salaam.

Kutokana na hali hiyo ameomba Mahakama wapewe wiki mbili kwa ajili ya kuhakikisha DPP analifanyia kazi hata kama atakuwa Dodoma watamfuata huko huko.Baada ya Hakimu Swai kueleza hayo, Aveva aliomba wapewe muda wa siku saba kwa sababu siku 14 ni nyingi na kuongeza kuwa upande wa mashtaka wanavyochelewesha jambo hilo wanawaumiza.

Pia Nyange ameongeza kuwa jambo hilo la kubadilisha hati ya mashtaka kwa kuwaondoa washtakiwa hao ni la muda wa zaidi ya miezi miwili wakati wanajua wapo mahabusu kwa zaidi ya mwaka mmoja na kuendelea kukaa huko ni tatizo.Amesisitiza kuwa kuendelea kuwapatia upande wa mashtaka wiki mbili ni kama kuendelea kuwaficha Keko bila sababu za msingi.

Baada ya malalamiko hayo ya washtakiwa Hakimu Simba alimuuliza Wakili Swai unaona malalamiko ya washtakiwa hayana msingi. Swai akamjibu Hakimu Simba kuwa malalamiko yao yanamsingi mheshimiwa.Hakimu Simba unasemaje na afya ya mshtakiwa wa kwanza Aveva inaonekana ana kliniki kila wiki hivyo anawapa siku saba wakamilishe taratibu. Kesi imeahirishwa hadi Agosti 17 mwaka 2018

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 10 yakiwemo ya kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi, kutoa maelezo ya uongo na utakatishaji fedha haramu.


Hivyo makala UPANDE WA MASHTAKA WAPEWA SIKU SABA KUKAMILISHA MCHAKATO KUBADILI HATI YA MASHTAKA KESI YA AKINA AVEVA, NYANGE

yaani makala yote UPANDE WA MASHTAKA WAPEWA SIKU SABA KUKAMILISHA MCHAKATO KUBADILI HATI YA MASHTAKA KESI YA AKINA AVEVA, NYANGE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UPANDE WA MASHTAKA WAPEWA SIKU SABA KUKAMILISHA MCHAKATO KUBADILI HATI YA MASHTAKA KESI YA AKINA AVEVA, NYANGE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/upande-wa-mashtaka-wapewa-siku-saba.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "UPANDE WA MASHTAKA WAPEWA SIKU SABA KUKAMILISHA MCHAKATO KUBADILI HATI YA MASHTAKA KESI YA AKINA AVEVA, NYANGE"

Post a Comment