Twanga Pepeta kusheherekea miaka 20 Septemba 29

Twanga Pepeta kusheherekea miaka 20 Septemba 29 - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Twanga Pepeta kusheherekea miaka 20 Septemba 29, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Twanga Pepeta kusheherekea miaka 20 Septemba 29
kiungo : Twanga Pepeta kusheherekea miaka 20 Septemba 29

soma pia


Twanga Pepeta kusheherekea miaka 20 Septemba 29

Dar es Salaam. Bendi kongwe nchini, The African Stars (Twanga Pepeta) imeandaa onyesho maalum la kutimiza miaka 20 tokea kuanzishwa kwake Septemba 29.

Bendi hiyo iliyoanzishwa mwaka 1998, itafanya onyesho lake kwenye ukumbi wa Club Legends uliopo Namanga na maandalizi yake yameanza.

Mkurugenzi wa bendi hiyo, Asha Baraka alisema kuwa sambamba na onyesho hilo, shughuli mbalimbali zitafanywa na wanamuziki wa bendi hiyo ikiwa pamoja na kutembelea ofisi za vyombo vya habari mbalimbali, kusaidia watoto yatima na wagonjwa.Baraka alisema kuwa kudumu kwa miaka 20 katika muziki wa dansi si kazi ndogo kwani kuna bendi nyingi zilizoanzishwa baada ya bendi yao kuanzishwa zimeshindwa kuendelea na shughuli za muziki. Bendi hiyo ilifanikiwa kuzindua albamu 14.

Alisema kuwa bendi yao imepitia changamoto nyingi kwa kipindi chote hicho ikiwa pamoja na kupanda na kushuka, lakini uongozi wa kampuni inayomiliki bendi hiyo, African Stars Entertainment Tanzania (Aset) ilisimama kidete kuhakikisha wanadumu katika soko la muziki tofauti na bendi nyingine.

“Miaka 20 si midogo kudumu katika shughuli za muziki, kwa kweli tumepitia changamoto nyingi sana, wanamuziki kuhama, soko la muziki wa dansi kushuka kutokana na mabadiliko ya sekta hiyo ikiwa pamoja na kuibuka kwa muziki wa kizazi kipya (bongo fleva), taarab na Singeli. Mashabiki walibadili muelekeo, lakini sasa mambo yamerejea,” alisema Baraka.

Alisema kuwa kwa miaka hiyo 20, wameweza kupata mafanikio mbalimbali ikiwa pamoja na kuanzisha bendi nyingine kama African Revolution enzi ya Chumvi Chumvi mpaka Tam Tam na baadaye kubadilishwa jina na kuwa Vibration Sound.

“Pia tuliweza kuanzisha studio (Aset Production), gazeti (Zeze), kituo cha kuibua vipaji (Aset Academia) na kuibua wanamuziki nyota kama Totoo Kalala ambaye kwa sasa anatamba na bendi ua Bogos ya Musica na wanamuziki wengine wengi sana,” alisema.Alifafanua kuwa pia waliwekeza katika sekta ya filamu na kufanya kazi na waigizaji mbalimbali nchini ikiwa pamoja na marehemu, Steven Kanumba na wengineo huku wakisaidia wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya kupata maonyesho ya nje kama Uingereza na nchi nyinginezo.

“Bendi yenyewe ilifanya maonyesho nje ya nchi mbalimbali za Scandinavia kama Norway, Sweden, Denmark na Finland, pia bendi ilifanya maonyesho kadhaa nchini Uingereza na kushiriki katika tamasha la mfalme wa Oman,” alisema.
Mkurugenzi wa bendi ya African Stars (Twanga Pepeta), Asha Baraka (wanne kutoka kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana sherehe maalum ya miaka 20 ya bendi hiyo iliyopangwa kufanyika kwenye ukumbi wa Le Legends Septemba 26. Picha na Mwandishi wetu.


Hivyo makala Twanga Pepeta kusheherekea miaka 20 Septemba 29

yaani makala yote Twanga Pepeta kusheherekea miaka 20 Septemba 29 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Twanga Pepeta kusheherekea miaka 20 Septemba 29 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/twanga-pepeta-kusheherekea-miaka-20.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Twanga Pepeta kusheherekea miaka 20 Septemba 29"

Post a Comment