title : TPA KUHUDUMIA TANI MILIONI I4
kiungo : TPA KUHUDUMIA TANI MILIONI I4
TPA KUHUDUMIA TANI MILIONI I4
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inatarajia kuhudumia tani 14,374,400 yakiwemo makontena (TEUs) 208,000 katika vitengo vinavyoendeshwa na mamlaka hiyo kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019.
Kitengo cha Kontena katika Bandari ya Dar es Salaam (TICTS) pia kinatarajia kuhudumia makontena (TEUs) 489,300 katika mwaka huo wa fedha.
Mkurugenzi Mkuu wa (TPA), Deusdedit Kakoko amesema hayo Dar es Salaam wakati akielezea mpango na bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019 ya mamlaka hiyo.
"Tunatarajia kukusanya mapato ya jumla ya Sh bilioni 1,012.586, matumizi ni Sh bilioni 778.297 na kupata ziada ya Sh bilioni 234.289," amesema.
Pia alisema wanatarajia kuhudumia meli 2,736 zenye ukubwa wa (GRT) milioni 35.880 na kati ya hizo meli 1,307 ni za Kimataifa (Deep Sea), meli 786 ni za mwambao na meli 670 zitahudumiwa katika bandari za Maziwa.
Kakoko alisema, wataimarisha mfumo na kuongeza matumizi ya Tehama kwa malipo kwa kutumia mtandao (e-payment) na kukamilisha mradi na kutumia mfumo mpya wa 'Enterprise Resource Planning'(ERP) katika kutoa huduma na ukusanyaji wa mapato.
Aidha amesema watakusanya mapato kwa wakati na kuziba mianya yote ya upotevu wa mapato na kukusanya kwa kupitia benki sambamba na kuzingatia matumizi ya 'flow meters' na skana katika kuhakikisha shehena ya mafuta na shehena kwenye kontena.
"Tumejiwekea mikakati ya kuvutia shehena kwa kuboresha huduma za mamlaka kwa kutekeleza miradi mbalimbali kwa wakati uliopangwa sambamba na kuimarisha ulinzi na usalama katika bandari za Mamlaka," amesema.
Hivyo makala TPA KUHUDUMIA TANI MILIONI I4
yaani makala yote TPA KUHUDUMIA TANI MILIONI I4 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TPA KUHUDUMIA TANI MILIONI I4 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/tpa-kuhudumia-tani-milioni-i4.html
0 Response to "TPA KUHUDUMIA TANI MILIONI I4"
Post a Comment