title : TABORA KUZINDUA KAMPENI YA FURAHA YANGU MJINI NZEGA SIKU YA IJUMAA
kiungo : TABORA KUZINDUA KAMPENI YA FURAHA YANGU MJINI NZEGA SIKU YA IJUMAA
TABORA KUZINDUA KAMPENI YA FURAHA YANGU MJINI NZEGA SIKU YA IJUMAA
NA TIGANYA VINCENT
TABORA
MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri anatarajia kuzindua rasmi kampeni ya kimkoa ya upimaji virusi vya Ukimwi VVU inayojulikana kwa jina la ‘Furaha Yangu’ yenye lengo la kuhamasisha huduma za kupima VVU na kuanza ARV mapema hasa kwa wanaume.
Kampeni hiyo itakayozinduliwa Agosti 3 mwaka huu mjini Nzega, inalenga kuwaleta wanaume kwenye huduma kutokana na wengi wao kuwa waoga kuzifikia.
Kaimu Mganga MKuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Kevin Nyakimori alisema kampeni hiyo inahamasisha mkakati mpya wa Serikali wa upimaji wa VVU na kuanza kutumia ARV mapema kwa wale watakaokutwa na VVU.
Alisema lengo lake ni kuchochea mabadiliko ya tabia ndani ya jamii ili kuongeza idadi ya Watanzania walio katika mazingira hatarishi wajitokeze kupima na kujua hali za afya zao katika suala zima la VVU.
Dkt Nyakimori alisema kampeni hiyo itazinduliwa katika viwanja wa Parking mjini Nzega na itakuwa na siku mbili za kutoa huduma za afya bila malipo ikiwemo huduma ya upimaji wa VVU kuanzia Agosti 3 hadi tarehe 4 Mwezi huu.
Alisema kampeni hiyo ni muhimu kwa Mkoa huo kwani matokeo yanaonyesha kiwango cha maambukizi ni asilimia 5.1 kwa watu wenye umri kati ya miaka 15 hadi 49 ambacho ni kiwango cha juu ya kile cha kitaifa 4.7.
Kaimu Mganga huyo wa Mkoa alisema juhudi za serikali ni kufikia malengo ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Ukimwi (UNAIDS) ni kutaka kutambua watu wote wanaoishi na VVU kutambua hali zao na watue ARV ili waweze kufubaza virusi hivyo
Dkt. Nyakimori alizitaja huduma ambazo zitatolewa ni upimaji wa VVU, huduma za uzazi wa mpango, uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi na matiti, uchunguzi wa maambukizi ya kifua kikuu , uchunguzi wa magonjwa yasiyo ambukizwa na uchangiaji damu.
Hivyo makala TABORA KUZINDUA KAMPENI YA FURAHA YANGU MJINI NZEGA SIKU YA IJUMAA
yaani makala yote TABORA KUZINDUA KAMPENI YA FURAHA YANGU MJINI NZEGA SIKU YA IJUMAA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TABORA KUZINDUA KAMPENI YA FURAHA YANGU MJINI NZEGA SIKU YA IJUMAA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/tabora-kuzindua-kampeni-ya-furaha-yangu.html
0 Response to "TABORA KUZINDUA KAMPENI YA FURAHA YANGU MJINI NZEGA SIKU YA IJUMAA"
Post a Comment