title : SIMBA KUMKOSA BOCCO JUMAMOSI
kiungo : SIMBA KUMKOSA BOCCO JUMAMOSI
SIMBA KUMKOSA BOCCO JUMAMOSI
Taarifa kutoka Simba zinasema kuna uwezekano mkubwa wa kumkosa nahodha wake, John Bocco katika mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Mtibwa Sugar unaotarajiwa kuchezwa katika Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, Agosti 18.
Akizungumza jana, Daktari wa Simba, Yasin Gembe, alisema Bocco bado ni majeruhi na amekosa mechi mbili za kirafiki. “Hali ya Bocco haijatengemaa, naendelea kumhudumia nione kama anaweza kucheza mchezo wa ngao ya hisani kwani amekosa michezo miwili,” alisema Gembe.
Bocco alikosa mchezo wa kirafiki dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana Agosti 8 katika tamasha la Simba Day, ambao lilimalizika kwa sare ya bao 1-1 na juzi dhidi ya Namungo FC huko Ruangwa, Lindi walitoka suluhu.
Presha imeanza kuwa kubwa kwa Simba kwani licha ya kutumia kiasi kikubwa cha fedha kusajili na kuweka kambi nchini Uturuki, hawajapata ushindi katika michezo miwili iliyochezwa hapa nyumbani.
Baada ya mchezo wa Ngao Jamii utakaofanyika Jumamosi, Simba itafungua dimba Agosti 22 kwa kuwakaribisha wajeda wa Magereza ‘Tanzania Prisons’ kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Chanzo:habari leo.
Hivyo makala SIMBA KUMKOSA BOCCO JUMAMOSI
yaani makala yote SIMBA KUMKOSA BOCCO JUMAMOSI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SIMBA KUMKOSA BOCCO JUMAMOSI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/simba-kumkosa-bocco-jumamosi.html
0 Response to "SIMBA KUMKOSA BOCCO JUMAMOSI"
Post a Comment