RPC TEMEKE ATOA UFAFANUZI SAKATA LA NDUGU KUSUSA KUZIKA.

RPC TEMEKE ATOA UFAFANUZI SAKATA LA NDUGU KUSUSA KUZIKA. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RPC TEMEKE ATOA UFAFANUZI SAKATA LA NDUGU KUSUSA KUZIKA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RPC TEMEKE ATOA UFAFANUZI SAKATA LA NDUGU KUSUSA KUZIKA.
kiungo : RPC TEMEKE ATOA UFAFANUZI SAKATA LA NDUGU KUSUSA KUZIKA.

soma pia


RPC TEMEKE ATOA UFAFANUZI SAKATA LA NDUGU KUSUSA KUZIKA.

Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Emmanuel Mkula ametoa ufafanuzi kuhusu na sakata la ndugu kugoma kumzika ndugu yao ambaye mwili wake kwa sasa upo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Agosti II mwaka huu Marehemu Kindamba akiwa wenzake watatu maeneo ya Kiwalani katika Mgahawa wa Clouds Motel alipigwa risasi wakati akijaribu kuwatoroka askari waliokwenda kuwakamata kwa ajili ya kuhojiwa baada kupatikana taarifa wanadhaniwa ni majambazi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam RPC Mkula amesema kuwa Agosti II mwaka  majira ya saa I0 jioni mkuu wa upelelezi wilaya ya chang'ombe alipokea taarifa kuna watu wanaodhaniwa ni majambazi katika hoteli ya Clouds.

Amesema kuwa baada ya kujiridhisha na taarifa hiyo walifika eneo la tukio na kuwakuta watu wanne wakiwa katika mgahawa.

RPC Mkula amefafanua kuwa baada ya askari kujitambulisha kwa watu hao, mmoja kati ya watuhumiwa hao Salum Juma Kindamba alikurupuka na hukimbia huku akiwa ameshikiria mfuko mkoni ambao askari walidhani kuna bastola.

"Askari walifyatua risasi hewani kumwashiria asimame lakini alikaidi amri na kuendelea kukimbia ili kufanikisha ukamataji askari alifyatua risasi iliyomjeruhi kiunoni na mguuni na kudondoka chini" amesema RPC Mkula.

RPC Mkula ameeleza kuwa baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo na kumkagua walifanikiwa kukuta fedha  tisa pamoja na simu aina ya Tecno.

"Baada hapo majeruhi alipelekwa hospitali ya Rufaa Mkoa wa Temeke kwa matibabu zaidi lakini baadaye alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu" RPC Mkula.

Ameeleza kuwa upelelezi wa awali inaonyesha watuhumiwa hao wanajihusisha na vitendo vya kiuhalifu ndio maana marehemu alikimbia baada ya kuwaona polisi.

"Ndugu wa marehemu walikabidhiwa mwili kwa ajili ya mazishi ni Omary S/O Juma Kindamba pamoja na Alfan S/O Kindamba" amesema RPC Mkula.

RPC Mkula amesema kwa mara kadhaa kumekuwa na matukio ya ujambazi na uporaji wa kutumia silaha ambapo baada kukithiri kwa vitendo hivyo, Kamanda wa Kanda Maalum ya DSM, Lazaro Mambosasa akatoa maagizo kwa Makamanda wa polisi wa mikoa ya kipolisi mitatu, Ilala, Kinondoni kuandaa kikosi kazi cha kupambana na majambazi.

RPC Mkula amewataja watuhumiwa hao ni Moses Benjamini Halamela (30) na Omary Huseini Mhando (33) wakazi wa Kimara Temboni pamoja na Agape Kalyembe Mwakanyamale (34) mkazi wa Kitunda Kinyantira.






Hivyo makala RPC TEMEKE ATOA UFAFANUZI SAKATA LA NDUGU KUSUSA KUZIKA.

yaani makala yote RPC TEMEKE ATOA UFAFANUZI SAKATA LA NDUGU KUSUSA KUZIKA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RPC TEMEKE ATOA UFAFANUZI SAKATA LA NDUGU KUSUSA KUZIKA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/rpc-temeke-atoa-ufafanuzi-sakata-la.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "RPC TEMEKE ATOA UFAFANUZI SAKATA LA NDUGU KUSUSA KUZIKA."

Post a Comment