RC MAKONDA ALAANI MGAMBO KUMSHAMBULIA RAIA,AAGIZA AKAMATWE

RC MAKONDA ALAANI MGAMBO KUMSHAMBULIA RAIA,AAGIZA AKAMATWE - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RC MAKONDA ALAANI MGAMBO KUMSHAMBULIA RAIA,AAGIZA AKAMATWE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RC MAKONDA ALAANI MGAMBO KUMSHAMBULIA RAIA,AAGIZA AKAMATWE
kiungo : RC MAKONDA ALAANI MGAMBO KUMSHAMBULIA RAIA,AAGIZA AKAMATWE

soma pia


RC MAKONDA ALAANI MGAMBO KUMSHAMBULIA RAIA,AAGIZA AKAMATWE

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akizungumza na MICHUZI BLOG leo jijini Dar es Salaam.

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema amesikitishwa na kitendo cha mgambo kumshambulia kijana Robson Orotho(41)mkazi wa Bunju B kwa sababu za kutolipa faini ya usafi.

Ametaka mgambo huyo ambaye amehusika na tukio hilo akamatwe na kuchukuliwa hatua na kusisitiza kitendo hicho ni cha kinyama na anakilaani.

Makonda amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza kwenye mahojiano maalum na MICHUZI BLOG kuhusu video inayosambaa ikionesha kijana huyo akishambuliwa kwa rungu kwa kupigwa miguuni.

Mbali na video hiyo,pia MICHUZI BLOG ilitaka kufahamu hatua gani ambazo anachukua kutokana na mgambo hao kushambulia na kupiga wananchi katika kutekeleza agizo la kusimamia usafi.

Hivyo Makonda amesema kuwa anasikitishwa na tukio la kushambuliwa kwa mkazi huyo wa Bunji B jijini na kwamba tayari ameagiza kwa Kamanda wa Kanda Malaaum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa kuhakikisha mgambo huyo anakamatwa.

Pia amesema dhana ya kuwatumia mgambo na JKT kufanya usafi ilikuwa njema na kufafanua mgambo hao wamekabidhiwa kwenye Serikali za mitaa na hivyo watendaji wanapaswa kusimamia.

Amesema inasikitisha kuona badala ya kutoza faini wanashambulia na kupiga watu na kwamba kumpiga mtu ni sawa na kumpa adhabu.

Ameongeza kuwa katika kuhakikisha suala la usafi linafanyika kwa misingi ya haki waliweka utaratibu wa kutoza faini na si kupiga raia.

Makonda ameomba radhi kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na kusisitiza tukio hilo limemshitua na kufafanua hayo si makusudio ya awamu ya tano.

Hata hivyo amesema watawahoji watendaji ambao wanawajibika moja kwa moja kuhakikisha kanuni na taratibu zinafuatwa ili kupata ukweli kama watendaji hao wanatimiza majukumu yao kikamilifu.

Kwa upande wa Kamanda Lazaro Mambosasa alipotafutwa na MICHUZI BLOG  ili kufahamu kama mgambo aliyeonekana kwenye video hiyo kazm amekamatwa alijibu kwa kifupi hajakamatwa na akipatikana atakamatwa.

Hata hivyo taarifa kutoka Mkoa wa Polisi wa Kinondoni jijini Dar es Salaam zinaeleza tayari watu watatu wamekamatwa kutokana na tuhuma za kumashambulia mtu huyo.

Watu hao ni Kelvin Edson, Godluck Festo na Rehema Nyange ambao wote ni askari Mgambo wilaya ya Kinondoni.


Hivyo makala RC MAKONDA ALAANI MGAMBO KUMSHAMBULIA RAIA,AAGIZA AKAMATWE

yaani makala yote RC MAKONDA ALAANI MGAMBO KUMSHAMBULIA RAIA,AAGIZA AKAMATWE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RC MAKONDA ALAANI MGAMBO KUMSHAMBULIA RAIA,AAGIZA AKAMATWE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/rc-makonda-alaani-mgambo-kumshambulia.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "RC MAKONDA ALAANI MGAMBO KUMSHAMBULIA RAIA,AAGIZA AKAMATWE"

Post a Comment