title : RAIS MAGUFULI AHIMIZA WATENDAJI WA SERIKALI KUSIMAMIA ILANI YA CCM
kiungo : RAIS MAGUFULI AHIMIZA WATENDAJI WA SERIKALI KUSIMAMIA ILANI YA CCM
RAIS MAGUFULI AHIMIZA WATENDAJI WA SERIKALI KUSIMAMIA ILANI YA CCM
*Akumbusha Kafulila alivyoitwa Tumbili kwenye sakata la IPTL
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
RAIS Dk.John Magufuli amewataka viongozi wa ngazi mbalimbali nchini kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kikamilifu na kusimamia vema utekelezaji wa Ilani.
Amesema kuna watendaji wa Serikali ambao wamekuwa wakidai hawawezi kufuata Ilani kwa madai ya kuwa wapo Neutral na kwamba katika hilo hakuna Neutral kwani lazina Ilani itekelezwe.
Dk.Magufuli ametoa kauli hiyo leo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa tukio la kuwaapisha wakuu wa mikoa, Makatibu wakuu,manaibu makatibu wakuu pamoja na makatibu tawala ambao aliwateua mwishoni mwa wiki iliyopita..
Hivyo baada ya kuwaapisha viongozi hao Rais Magufuli amehimiza utendaji kazi kwa viongozi wa ngazi mbalimbali ili kuwatumikia vema Watanzania.
Amesema kuwa nchi yetu idadi ya watu ni milioni 55 hivyo waliopata nafasi imetokana na mipango ya Mungu na si kwa matakwa yao.Ameongeza kila aliyekuwa kwenye nafasi atambue yupo hapo kwasababu Mungu ameeamua na hata yeye kuwa Rais ni mpango wa Mungu.
Hivyo amewataka viongozi wote kwa ngazi mbalimbali kuanzia juu mpaka chini kila mmoja kwa nafasi yake afahamu yupo hapo kwasababu Mungu ametaka iwe hivyo na lazima wafanye kazi.Wakati anahimiza utendaji kazi na ushirikiano ameeleza umuhimu wa watendaji wa Serikali kuisimamia na kuitekeleza Ilani ya uchaguzi mkuu.
Amefafanua kuna watendaji wa Serikali ambapo wakienda kutekeleza majukumu yao wanasema wao ni watendaji wa Serikali na wapo Neutral.Amewataka wafahamu watendaji wa Serikali wanatakiwa kutekeleza Ilani ya CCM na katika hill lazima watambue hakuba bahari ya Neutral."Mimi ni Rais ninayetokana na CCM ,Makamu wa Rais ni wa CCM na Waziri Mkuu pia anatokana na CCM,"amesema na Rais Magufuli na kufafanua kila mmoja lazima ashiriki kuitekeleza Ilani hiyo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>
Hivyo makala RAIS MAGUFULI AHIMIZA WATENDAJI WA SERIKALI KUSIMAMIA ILANI YA CCM
yaani makala yote RAIS MAGUFULI AHIMIZA WATENDAJI WA SERIKALI KUSIMAMIA ILANI YA CCM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RAIS MAGUFULI AHIMIZA WATENDAJI WA SERIKALI KUSIMAMIA ILANI YA CCM mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/rais-magufuli-ahimiza-watendaji-wa.html
0 Response to "RAIS MAGUFULI AHIMIZA WATENDAJI WA SERIKALI KUSIMAMIA ILANI YA CCM"
Post a Comment