title : RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA MAMIA YA WAKAZI WA CHATO MAZISHI YA DADA YAKE MAREHEMU MONICA MAGUFULI YALIYOFANYIKA LEO
kiungo : RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA MAMIA YA WAKAZI WA CHATO MAZISHI YA DADA YAKE MAREHEMU MONICA MAGUFULI YALIYOFANYIKA LEO
RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA MAMIA YA WAKAZI WA CHATO MAZISHI YA DADA YAKE MAREHEMU MONICA MAGUFULI YALIYOFANYIKA LEO
Dada wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aitwaye Monica Joseph Magufuli aliyefariki dunia Jumapili tarehe 19 Agosti, 1955 katika hospitali ya Bugando Jijini Mwanza amezikwa leo katika makaburi ya familia yaliyopo katika kijiji cha Mlimani, Wilaya ya Chato Mkoani Geita.
Misa Takatifu ya Mazishi ya Monica Joseph Magufuli ameongozwa na Askofu Jimbo Katoliki la Rulenge Mhashamu Severine Niwemugizi aliyeambatana na Maaskofu wengine saba, imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Marais Wastaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi, Mhe. Benjamin William Mkapa na Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo ni Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Mhe. Raila Amolo Odinga, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Ndg. Philip Mangula, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mawaziri, Wabunge, Viongozi Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Viongozi wa Madhehebu ya Dini, Viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wengine mbalimbali wa Mikoa, Wilaya, Taasisi, Idara na Kampuni.
Akisoma Wasifu wa Marehemu kwa niaba ya Familia, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Bw. Gerson Msigwa amesema marehemu Monica Joseph Magufuli alizaliwa tarehe 25 Novemba, 2018 na ni mtoto wa kwanza wa Mzee Joseph Marco Magufuli (ambaye ametangulia mbele za haki) na Mama Suzana Ngolo Magufuli ambaye yupo hai.
Msigwa amesema Monica ameacha Mme, watoto 9 na Wajukuu 25.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mama yake mzazi Suzana Magufuli wakati wakitoa heshma za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Dada yake Monica Magufuli nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshma za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Dada yake Monica Magufuli nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsaidia Mama yake mzazi Suzana Magufuli wakati wakuweka udongo ndani ya kaburi la Marehemu Dada yake Monica Magufuli nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka udongo ndani ya kaburi la Marehemu Dada yake Monica Magufuli nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa kanisani katika Misa takatifu ya kumuombea Marehemu Dada yake Monica Magufuli. Wengine katika picha ni Mama yake Suzana Magufuli, Stanslaus Lori Madulu(Mme wa marehemu) , Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga pamoja na viongozi mbalimbali wa Kiserikali.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>
Hivyo makala RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA MAMIA YA WAKAZI WA CHATO MAZISHI YA DADA YAKE MAREHEMU MONICA MAGUFULI YALIYOFANYIKA LEO
yaani makala yote RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA MAMIA YA WAKAZI WA CHATO MAZISHI YA DADA YAKE MAREHEMU MONICA MAGUFULI YALIYOFANYIKA LEO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA MAMIA YA WAKAZI WA CHATO MAZISHI YA DADA YAKE MAREHEMU MONICA MAGUFULI YALIYOFANYIKA LEO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/rais-dkt-magufuli-aongoza-mamia-ya.html
0 Response to "RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA MAMIA YA WAKAZI WA CHATO MAZISHI YA DADA YAKE MAREHEMU MONICA MAGUFULI YALIYOFANYIKA LEO"
Post a Comment