Idadi ya Wagonjwa waliopandikizwa Figo Muhimbili yafikia 19

Idadi ya Wagonjwa waliopandikizwa Figo Muhimbili yafikia 19 - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Idadi ya Wagonjwa waliopandikizwa Figo Muhimbili yafikia 19, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Idadi ya Wagonjwa waliopandikizwa Figo Muhimbili yafikia 19
kiungo : Idadi ya Wagonjwa waliopandikizwa Figo Muhimbili yafikia 19

soma pia


Idadi ya Wagonjwa waliopandikizwa Figo Muhimbili yafikia 19

Dar es salaam 21-08-2018 

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) inaendelea kutoa huduma ya kupandikiza figo ambapo hadi hivi sasa tayari wagonjwa 19 wamenufaika na huduma hiyo tangu ilipoanzishwa kwa mara ya kwanza hapa nchini Novemba mwaka 2017.

Utoaji wa huduma hiyo ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambayo ili elekeza kuweka mipango thabiti ya kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya matibabu ambayo yalikuwa hayatolewi hapa nchini ama kutokana na wataalam wa kutoa huduma hizo au vifaa vya uchunguzi.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Hedwiga Swai alipokua akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Prof. Lawrence Museru kuhusu upandikizaji figo.

“Tunapenda kuwafahamisha kuwa wagonjwa wote tuliowapandikiza figo pamoja na ndugu zao waliojitolea figo wanaendelea vizuri na shughuli zao kama kawaida. Hii inaonesha ni kwa kiwango gani huduma hii imefanikiwa tangu ilipoanzishwa Novemba mwaka jana ”. amesema Dkt Swai.

Akifafanua amesem zoezi hilo la upandikizaji figo limeshirikisha wataalamu wazalendo toka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali ya BLK, Taasisi ya Saifee iliyopo Mumbai India pamoja na Hospitali ya kimataifa ya Sakra ya nchini India.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Muhimbili Dkt. Hedwiga Swai( katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo, kuhusu maendeleo ya upandikizaji figo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, kushoto ni Daktari bingwa upasuaji wa mfumo wa mkojo Njiku Kim , kulia ni Daktari bingwa wa magonjwa ya figo Onesmo Kisanga. 
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Njiku Kim akiandaa figo kabla ya kupandikizwa kwa mgonjwa. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Mfumo wa Mkojo wa Muhimbili, Victor Sensa akishirikiana na Dkt. Kim kuaandaa figo kwa ajili ya kupandikizwa kwa mgonjwa mwingine. 
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mfumo wa Mkojo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt . Isaack Mlatie akitoa figo kwa ajili ya kupandikiza kwa mgonjwa mwenye tatizo la figo. Katikati ni daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mfumo wa Mkojo, Muhimbili, Dkt. Gabriel Mtaturu akishiriki katika upasuaji huo. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mfumo wa Mkojo kutoka Hospitali ya Kimataifa ya Sakra nchini India, Dkt. Girish Nelivigi akishirikiana na madaktari wa Muhimbili kufanya upasuaji huo.
Wataalamu wakiendelea na upasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). 
Wataalamu wa upasuaji wa mfumo wa mkojo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa upasuaji wa mfumo wa mkojo kutoka nchini India.



Hivyo makala Idadi ya Wagonjwa waliopandikizwa Figo Muhimbili yafikia 19

yaani makala yote Idadi ya Wagonjwa waliopandikizwa Figo Muhimbili yafikia 19 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Idadi ya Wagonjwa waliopandikizwa Figo Muhimbili yafikia 19 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/idadi-ya-wagonjwa-waliopandikizwa-figo.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Idadi ya Wagonjwa waliopandikizwa Figo Muhimbili yafikia 19"

Post a Comment