NAIBU JAJI MKUU KENYA MATATANI

NAIBU JAJI MKUU KENYA MATATANI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NAIBU JAJI MKUU KENYA MATATANI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NAIBU JAJI MKUU KENYA MATATANI
kiungo : NAIBU JAJI MKUU KENYA MATATANI

soma pia


NAIBU JAJI MKUU KENYA MATATANI

Naibu Jaji mkuu Kenya Philomena Mwilu amekamatwa na kushtakiwa kwa uhalifu katika mahakama mjini Nairobi.

Amekabiliwa na mashtaka ya kutumia vibaya mamlaka, na kukwepa kulipa ushuru.

ameachiliwa kwa dhamana ya thamani ya $50,000 na anatarajiwa kufika mahakamani Jumatano asubuhi.

Awali Mwilu alipelekwa katika makao ya idara ya uchunguzi wa uhalifu DCI kuhojiwa.

Ni kiongozi wa juu katika idara ya mahakama kuwahi kukamatwa katika operesheni ya serikali kukabiliana na rushwa nchini.

Muda mfupi baada ya kukamatwa, mwendesha mashtaka mkuu nchini Noordin Haji ameitisha mkutano wa dharura na waandishi wa habari kuhusu suala hilo.

ameeleza kwamba idara ya mahakama itafanya kazi tu iwapo maafisa wa mahakama watatumia nafasi zao kujitajirisha kwa kisingizio cha Wakenya.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, mwendesha mashtaka huyo ametaja kuwa kuna ushahidi wa kutosha kumshtaki Mwilu kwa mkosa yakiwemo kutumia vibaya mamlaka kujinufaisha binafsi.
Kampeni ya serikali kupambana na rushwa:

Ahadi kuu ya Rais Uhuru Kenyatta alipochaguliwa kwanza kuingia uongozini mnamo 2013 ilikuwa ni kupambana na rushwa.

Lakini wakosoaji wake wanaeleza kwamba kasi haijaridhisha ya kulishughulikia hilo.

Kwa muda mrefu wengi wanataja kwamba kuwakamata viongozi wajuu serikali wanaotuhumiwa kuhusika na rushwa ndio njia pekee ya kuondosha ukwepaji wa sheria

Mnamo 2016, Kenya ilielezwa kupoteza thuluthi moja ya bajeti yake ya serikali kutokana na rushwa kila mwaka.
Licha ya kwamba hatua kama hii ya kukamatwa kwa maafisa wa ngazi ya juu serikali ambayo inatazamwa kuwa ya kutotarajiwa katika kihistoria ya Kenya, baadhi wanaona kwamba hatua hii sio ya kushangaza.
Kumeshuhudiwa visa kadhaa vya maafisa wa serikali kukamatwa kutokana na kutuhumiwa katika kashfa za rushwa lakini hakuna aliyehukumiwa kufikia sasa.
Hata hivyo uchunguzi wa hivi karibuni na kesi zilizowasilishwa dhidi ya maafisa wakuu baadhi zinaoenakana kuwa na nafasi ya kubadili mtazamo wa vita hivyo nchini tangu kuwepo kwa rushwa ya Anglo Leasing.


Hivyo makala NAIBU JAJI MKUU KENYA MATATANI

yaani makala yote NAIBU JAJI MKUU KENYA MATATANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU JAJI MKUU KENYA MATATANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/naibu-jaji-mkuu-kenya-matatani.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "NAIBU JAJI MKUU KENYA MATATANI"

Post a Comment