Mradi wa kutoa elimu ya matumizi ya mitandao kwa wanawake waanzishwa

Mradi wa kutoa elimu ya matumizi ya mitandao kwa wanawake waanzishwa - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mradi wa kutoa elimu ya matumizi ya mitandao kwa wanawake waanzishwa, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mradi wa kutoa elimu ya matumizi ya mitandao kwa wanawake waanzishwa
kiungo : Mradi wa kutoa elimu ya matumizi ya mitandao kwa wanawake waanzishwa

soma pia


Mradi wa kutoa elimu ya matumizi ya mitandao kwa wanawake waanzishwa

Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Women at Web Tanzania imezindua mradi maalumu wenye lengo la kutoa mafunzo ya matumizi ya mitandao ili kuongeza uwepo wa kundi hili mitandaoni.

Mradi huo unaofadhiliwa na Shirika la DW Akademie la nchini Ujerumani una lengo la kuhamasisha matumizi bora ya mitandao ikiwamo kuongeza  mijadala ya maendeleo kwa wanawake katika mitandao.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi huo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, mmoja wa viongozi wa mradi huo Carol Ndosi amesema kwamba moja ya shughuli zitakazofanyika katika uhamasishaji huo ni mafunzo kwa wanawake yanayohusu njia za kujilinda na vurugu za mitandao, kutambua fursa zilizopo mitandaoni pamoja na mambo mengine.

Alisema kuwa kwa sasa Tanzania hakuna takwimu zilizo wazi za udhalilishaji wa wanawake kwenye mitandao japokuwa wengi waliopo wameshakutana na aina ya udhalilishaji kwenye mitandao, hasa ya kijamii.
“Idadi ya watu wanaomiliki smart phone inaongezeka hivyo kuongeza hatari za wanawake kuwa wahanga wa unyanyasi katika platform hizo, kwa hiyo kupitia mradi huu, pamoja na kuhamasisha wanawake kuongezeka kutumia hii mitandao, tutawapatia mafunzo ya namna ya kujilinda ama kutambua wale wanataka kuwafanyia ukatili.

“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa kwa kuwa bado tuna ‘gap’ kubwa sana la wanawake kushiriki katika mijadala ya maendeleo nje ya mitandao, basi watumie fursa za mitandao kushiriki mijadala hiyo na kujiletea maendeleo,” alisema Ndosi.
Kwa kuanzia, mradi huo utaendesha mafunzo katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na pia kwa upande wa Zanzibar.



Hivyo makala Mradi wa kutoa elimu ya matumizi ya mitandao kwa wanawake waanzishwa

yaani makala yote Mradi wa kutoa elimu ya matumizi ya mitandao kwa wanawake waanzishwa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mradi wa kutoa elimu ya matumizi ya mitandao kwa wanawake waanzishwa mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/mradi-wa-kutoa-elimu-ya-matumizi-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mradi wa kutoa elimu ya matumizi ya mitandao kwa wanawake waanzishwa"

Post a Comment