Mkurugenzi Mkuu NSSF amtaka Mkandarasi kumaliza barabara Kigamboni kwa wakati.

Mkurugenzi Mkuu NSSF amtaka Mkandarasi kumaliza barabara Kigamboni kwa wakati. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mkurugenzi Mkuu NSSF amtaka Mkandarasi kumaliza barabara Kigamboni kwa wakati., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mkurugenzi Mkuu NSSF amtaka Mkandarasi kumaliza barabara Kigamboni kwa wakati.
kiungo : Mkurugenzi Mkuu NSSF amtaka Mkandarasi kumaliza barabara Kigamboni kwa wakati.

soma pia


Mkurugenzi Mkuu NSSF amtaka Mkandarasi kumaliza barabara Kigamboni kwa wakati.


Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF William Erio ametembelea daraja la Kigamboni kukagua maendeleo ya ujenzi wa kipande cha barabara ya lami yenye urefu wa Kilomita mbili inayo unganisha daraja la Nyerere na barabara ya Feri - Kibada iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Akikagua barabara hiyo mwishoni mwa wiki, William Erio amemtaka Mkandarasi CRJE kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo kwa haraka na kuhakikisha gharama ya ujenzi hazizidi kiasi cha gharama kilicho kubaliwa kwenye mkataba wa ujenzi kati ya NSSF na Mkandarasi huyo.

Kwa upande wa Mkandarasi amepokea maelezo ya Mkurugenzi Mkuu na kuahidi kutekeleza ujenzi huo. Pamoja na kuahidi utekelezaji, Mkandarasi ameomba nyongeza ya muda kutokakana na changamoto za kupatikana kwa malighafi ya udongo hasa ile ya G15.

Gharama ya mradi huu ni Tsh 21.3 billioni ambao unahusisha ujenzi wa barabara yenye njia sita, tatu kila upande zenye urefu wa kilomita mbili kutoka mwisho wa daraja hadi kwenye makutano ya barabara ya Fery - Kibada.

Pia, ujenzi unajumuisha mzunguko wenye mita za mraba 5,762, mifereji ya maji taka na yale ya mvua, kingo za katikati ya barabara "new jersey barriers", kalavati nne za umbo la boksi na moja ya ya umbo la bomba.
Sehemu ya kipande cha barabara unganishi kutoka mwisho wa daraja upande wa Kigamboni kuelekea barabara ya Fery - Kibada.Kaimu Meneja wa Miradi NSSF Abdon Mhando (wa pili kushoto), akitoa maelezo ya utekelezaji wa mradi kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF William Erio (wa kwanza kushoto), wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi wa NSSF Bw. Gabriel Silayo.


Hivyo makala Mkurugenzi Mkuu NSSF amtaka Mkandarasi kumaliza barabara Kigamboni kwa wakati.

yaani makala yote Mkurugenzi Mkuu NSSF amtaka Mkandarasi kumaliza barabara Kigamboni kwa wakati. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mkurugenzi Mkuu NSSF amtaka Mkandarasi kumaliza barabara Kigamboni kwa wakati. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/mkurugenzi-mkuu-nssf-amtaka-mkandarasi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mkurugenzi Mkuu NSSF amtaka Mkandarasi kumaliza barabara Kigamboni kwa wakati."

Post a Comment