MKURUGENZI AWATUPIA LAWAMA WAZAZI RORYA, KUMALIZA KESI ZA MIMBA KIENYEJI.

MKURUGENZI AWATUPIA LAWAMA WAZAZI RORYA, KUMALIZA KESI ZA MIMBA KIENYEJI. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MKURUGENZI AWATUPIA LAWAMA WAZAZI RORYA, KUMALIZA KESI ZA MIMBA KIENYEJI., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MKURUGENZI AWATUPIA LAWAMA WAZAZI RORYA, KUMALIZA KESI ZA MIMBA KIENYEJI.
kiungo : MKURUGENZI AWATUPIA LAWAMA WAZAZI RORYA, KUMALIZA KESI ZA MIMBA KIENYEJI.

soma pia


MKURUGENZI AWATUPIA LAWAMA WAZAZI RORYA, KUMALIZA KESI ZA MIMBA KIENYEJI.


Na Frankius Cleophace Rorya.

Mkurugenzi wa Halmashgauri ya Wilaya ya Rorya Mkoani Mara Charles Chacha ametupia lawana wazazi na walezi wilayani humo kwa kumaliza suala la kesi zinazohusu mimba kienyeji huku wakishawishi watoto wao kusema uongo jambo ambalo linakwamisha ushaidi ili kuwatia hatiani watuhumiwa kwa lengo la kumaliza changamoto hiyo.

Akijibu hoja ya diwani viti maalum kata ya Robour Diana Charles kuhusu suala la waischana kupata mimba na kukatisha masomo yao, Mkurugenzi amesema kuwa kesi zipo lakini chagamoto kubwa ni wazazi na walezi kumaliza kesi zao na watumiwa kienyeji jambo ambalo linapoteza ushaidi ili polisi waweze kuendelea na kesi hiyo kwa lengo la kuwatia hatiani watuhumiwa hao.

“Binti akiletwa polisi kuhojiwa anaambiwa na mzazi kuwa aseme alikutana na mwanaume sokoni akampa mimba kweli kwa kawaida mtu ukutane nae siku ya soko apo apo uwe na mahusiano akupatie ujauzito siyo kweli hivyo sasa wazazi na madiwani tushilikiane vyema kutokomeza suala hilo pia wazazi waondokane na suala la kumaliza kesi wenyewe jambo hilo linapoteza ushaidi na watoto wetu wanazii kuangamia ” alisema Charles.

Akichangia hoja diwani wa viti maalum kata ya Rabour Diana Charles amesema kuwa Mikakati ambayo iliwekwa kipindi cha Nyuma takwimu za watoto kupata mimba zilishuka lakini kwa awamu hii ya robo ya tatu takwimu zimepanda tena ambapo watoto 18 wa shule za msingi na sekondari wilayani humo wamesitisha masomo kwa kupatiwa Ujauzito hivyo amesema kuwa kuna haja kubwa ya kuendeleza mikakati ya awali ili kupunguza takwimu hizo.

Naye diwani wa kata ya Nyamagaro Ezra Masana amependekeza kuwa maofisa elimu sekondari na msingi ngazi ya kata wachukue jukumu la kufuatilia masuala ya mimbo kwa watoto wa shule na siyo jukumu hilo kuwaachia maofisa watendaji wa kata.“Ili jukumu la kufuatilia watuhumiwa wanaowapa watoto wetu mimba sasa maofisa elimu msingi na sekondari waweke mkazo na siyo kuwaachia jukumu hili watendaji wa kata kila mara wako mahakamani na kushindwa kufanya shughuli za utendaji” alisema Masana.

Akichangia katika Sekta ya Elimu Diwani wa kata ya Koryo Peter Sarungi anabainisha kuwa suala la wanafunzi wa Shule za Msingi kutokujua kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) bado ni changamoto katika baadhi ya shule za msingi wilayani humo hivyo Madiwani wamesisitizwa kuleta taarifa hizo kwenye baraza la madiwani ili ziwezekufanyiwa kazi.

“Kuna baadhi ya kata wamelta taarifa hizo zimo kwenye vitabu lakini wengine hawajaleta na mimi nilifanya ziara na kamati ya Elimu Afya na Maji lakini kuna baadhi ya shule wanafuzi zaidi ya Miambili darasa la kwanza mpaka la tatu hawajui KKK” alisema Peter.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya Charles Chacha akisistiza suala watoto kupatiwa ujauzito amabapo anazidi kulaumu wazazi na walezi wilayani humo kumaliza kesi kienyeji na kusababisha kupotea kwa ushaidi ili kuwatia hatiani watuhumiwa.


Hivyo makala MKURUGENZI AWATUPIA LAWAMA WAZAZI RORYA, KUMALIZA KESI ZA MIMBA KIENYEJI.

yaani makala yote MKURUGENZI AWATUPIA LAWAMA WAZAZI RORYA, KUMALIZA KESI ZA MIMBA KIENYEJI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MKURUGENZI AWATUPIA LAWAMA WAZAZI RORYA, KUMALIZA KESI ZA MIMBA KIENYEJI. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/mkurugenzi-awatupia-lawama-wazazi-rorya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MKURUGENZI AWATUPIA LAWAMA WAZAZI RORYA, KUMALIZA KESI ZA MIMBA KIENYEJI."

Post a Comment