title : MFANYABIASHARA AMZAWADIA RC MTAKA KUTAMBUA MCHANGO WAKE KWENYE MAENDELEO YA UCHUMI WA SIMIYU
kiungo : MFANYABIASHARA AMZAWADIA RC MTAKA KUTAMBUA MCHANGO WAKE KWENYE MAENDELEO YA UCHUMI WA SIMIYU
MFANYABIASHARA AMZAWADIA RC MTAKA KUTAMBUA MCHANGO WAKE KWENYE MAENDELEO YA UCHUMI WA SIMIYU
Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akipokea zawadi ya unga wa ngano, mafuta ya kula na sukari, kutoka kwa Elizabeth Mlanda (kulia) mke wa Mfanyabiashara Clement Mlanda wa Mjini Bariadi, Agosti 04, 2018, ikiwa ni shukrani yake kwa kutambua mchango wa Mkuu huyo wa Mkoa katika maendeleo ya Uchumi wa mkoa wa Simiyu .
Elizabeth Mlanda(kulia) mke wa Mfanyabiashara Clement Mlanda akimkabidhi Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka bahasha yenye fedha kama shukrani yake kwa kutambua mchango wa Mkuu huyo wa Mkoa katika maendeleo ya Uchumi wa mkoa wa Simiyu .
Na Stella Kalinga, Simiyu
Bibi. Elizabeth Mlanda Mke wa Mfanyabiashara Mkubwa wa Mjini Bariadi mkoani Simiyu, Bw. Clement Mlanda Shigugulu ambaye anamiliki Hotel ya MS COMPLEX amemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka zawadi ya fedha taslimu (kiasi ambacho hakikutajwa), kilo 50 za sukari, kilo 25 za unga wa ngano na lita 40 za mafuta ya kula, ikiwa ni shukrani kwake kwa namna uongozi wake ulivyochangia kuufungua mkoa wa Simiyu kiuchumi na kuwawezesha wafanyabiashara wa mkoa huo kufanya biashara katika nyakati mbalimbali.
Amesema kupitia uongozi wa Mhe. Mtaka kumekuwa na matukio makubwa yanayochangia kuongezeka kwa mzunguko wa biashara mkoani Simiyu, ikiwemo Maonesho ya Kilimo na Sherehe za wakulima Nanenane ambayo yamewaleta watu kutoka sehemu mbalimbali hivyo kuwanufaiisha wafanyabiashara wa Simiyu hususani wamiliki wa hoteli na nyumba za kulala wageni.
" Jana nilienda Uwanja wa Nanenane nikakuta mambo mazuri, nilipokuja hotelini kwetu nako nikakuta watu wamejaa, nikamuuliza baba(mume wake) kuwa tutampa nini huyu Mkuu wa mkoa wetu kwa mambo mazuri anayotufanyia ya kutuletea maendeleo hivi na kutuletea heshima mkoa wetu mpya wa Simiyu " alisema.
"Nilimwambia mume wangu nitampa zawadi yoyote kumshukuru ili moyo wangu ufurahi, Nimemletea mafuta ndoo mbili za lita 20, sukari kilo 50,unga wa ngano kilo 25, nampongeza sana na Mungu amzidishie aendelee na moyo huu wa kutuletea maendeleo Mkoa wetu mpya wa Simiyu" alisisitiza Bibi. Elizabeth.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amemshukuru Mfanyabiashara huyo kwa zawadi hizo na akaeleza kuwa itakuwa ni kumbukumbu katika maisha yake huku akifafanunua kuwa kazi anayoifanya ni wajibu wake katika kuwaletea wananchi.
Ameongeza kuwa mikoa mingi imekuwa kiuchumi kutokana mchango wa viongozi waliopo, waliopita kwa kushirikiana na wananchi pamoja na wafanyabiashara.
"Maendeleo ndiyo nia ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kama ilivyokuwa kwa Marais, mawaziri waliopita, na kwa mkoa wa Simiyu mchango wangu unaendeleza kile walichofanya wakuu wenzangu wa mkoa walionitangulia, Marehemu Mabiti na baba yangu Elaston Mbwilo"'alisema.
Hivyo makala MFANYABIASHARA AMZAWADIA RC MTAKA KUTAMBUA MCHANGO WAKE KWENYE MAENDELEO YA UCHUMI WA SIMIYU
yaani makala yote MFANYABIASHARA AMZAWADIA RC MTAKA KUTAMBUA MCHANGO WAKE KWENYE MAENDELEO YA UCHUMI WA SIMIYU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MFANYABIASHARA AMZAWADIA RC MTAKA KUTAMBUA MCHANGO WAKE KWENYE MAENDELEO YA UCHUMI WA SIMIYU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/mfanyabiashara-amzawadia-rc-mtaka.html
0 Response to "MFANYABIASHARA AMZAWADIA RC MTAKA KUTAMBUA MCHANGO WAKE KWENYE MAENDELEO YA UCHUMI WA SIMIYU"
Post a Comment