title : MATUKIO KATIKA PICHA JUKWAA LA FURSA NA BIASHARA LINALOENDELEA MKAONI GEITA
kiungo : MATUKIO KATIKA PICHA JUKWAA LA FURSA NA BIASHARA LINALOENDELEA MKAONI GEITA
MATUKIO KATIKA PICHA JUKWAA LA FURSA NA BIASHARA LINALOENDELEA MKAONI GEITA
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe akitizama mvinyo uitwao (Perfect Wine) iliyoandaliwa kwa matunda ya nanasi iliyotengenzwa na kikundi cha Cris Food Products wa mkoani Geita alipokuwa akitembelea mabanda ya wafanyabiashara waliyoshiriki Jukwaa la Fursa za Biashara leo katika viwanja vya Gadeco,ambapo jukwaa hilo limeandaliwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) (pembeni kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe (wa kwanza kulia) akifurahia jambo na wenzake mara baada ya kupewa magazeti ya Habari Leo na Dailynews kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) alipokuwa akitembelea mabanda ya wafanyabiashara waliyoshiriki maonesho ya Jukwaa la Fursa za Biashara lililoandaliwa na (TSN) leo mkoani Geita katika viwanja vya Gadeco (wakwanza kushoto) ni Msemaji Mkuu wa Serikali Tanzania Dkt.Hassan Abbas na wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe (wa kwanza kulia) akizungumza na watendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhusu kusaidia wadau wa sekta ya filamu mkoa wa Geita kupatiwa Stika za TRA katika ofisi ya TRA mkoani hapo badala ya wasanii hao kulazimika kwenda mpaka ofisi za Dar es Salaam alipowatembea katika banda lao la Maonesho ya Jukwaa la Fursa za Biashara katika viwanja vya Gadeco,wakwanza kulia ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu ya Mlipa Kodi Bw.Richard Kayombo na katikati ni Meneja wa Ofisi ya TRA Mkoa wa Geita James Jilala.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe (wa kwanza kulia)akionyeshwa asali iliyopitishwa katika viwango vya kimataifa inayozalishwa katika wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita na mmoja wa wajasiriamali ambaye jina lake halikutambulika kwa harakaalipotembelea mabanda ya Maonesho ya wadau waliyoshiriki Jukwaa la Fursa za Biashara lililoandaliwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN).
Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya TSN Dkt.Hassan Abbas akitizama bidhaa za wajasiriamali waliyoshiriki Jukwaa la Biashara linalofanyika leo Mkoani Geita lililoandaliwa na (TSN ) katika maonesho yanayofanyika katika viwanja vya Gadeco Halmashauri ya Mkoa wa Geita.
Hivyo makala MATUKIO KATIKA PICHA JUKWAA LA FURSA NA BIASHARA LINALOENDELEA MKAONI GEITA
yaani makala yote MATUKIO KATIKA PICHA JUKWAA LA FURSA NA BIASHARA LINALOENDELEA MKAONI GEITA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MATUKIO KATIKA PICHA JUKWAA LA FURSA NA BIASHARA LINALOENDELEA MKAONI GEITA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/matukio-katika-picha-jukwaa-la-fursa-na.html
0 Response to "MATUKIO KATIKA PICHA JUKWAA LA FURSA NA BIASHARA LINALOENDELEA MKAONI GEITA"
Post a Comment