Makamu wa Pili wa Rais wa Zanziubar Balozi Seif Ali Iddi akaguwa Majengo mapya ya Skuli za Sekondari

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanziubar Balozi Seif Ali Iddi akaguwa Majengo mapya ya Skuli za Sekondari - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanziubar Balozi Seif Ali Iddi akaguwa Majengo mapya ya Skuli za Sekondari, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Makamu wa Pili wa Rais wa Zanziubar Balozi Seif Ali Iddi akaguwa Majengo mapya ya Skuli za Sekondari
kiungo : Makamu wa Pili wa Rais wa Zanziubar Balozi Seif Ali Iddi akaguwa Majengo mapya ya Skuli za Sekondari

soma pia


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanziubar Balozi Seif Ali Iddi akaguwa Majengo mapya ya Skuli za Sekondari

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanziubar Balozi Seif Ali Iddi alisema wakati Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inazidi  kuimarisha miundombinu ndani ya Sekta ya Elimu, Wanafunzi Nchini wanalazimika kujikita zaidi katika kutafuta Elimu itakayowajengea njia ya Maisha ya furaha wao na Familia zao.
Alisema wanafunzi hao wakiamua kusoma kwa juhudi na maarifa na kufikia kiwango cha Elimu ya juu ya Vyuo Vikuu watakuwa na nafasi pana ya kujihakikishia fursa za ajira zilizozoweya kufanywa na Wataalamu wa Kigeni.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akisalimiana na Wananchi wa Mwambe akiendelea na ziara yake ya kukaguwa Majengo mapya ya Skuli za Sekondari zinazojengwa kwa pamoja kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mshirika wa Maendeleo Mfuko wa Kimataifa wa Opec.
Alisema Taifa linahitaji kuwa na Wataalamu wake wenyewe  watakaotokana na Wanafunzi wake ambao watapaswa kuweka malengo ya kusoma kwa bidii kwa lengo la kuwahudumia Wananchi kwa kiwango cha uzalendo zaidi.
Balozi Seif alimuhimiza zaidi Mtoto wa Kike Nchini kusoma kwa ziada ili zile kazi za Kitaalamu zinazofanywa na Wanaume akatolea mfano za huduma za Afya wazifanye wenyewe katika azma ya kulinda na kuheshima mila, sila, Tamaduni na hata imani za Kidini.
Katika kutilia mkazo nafasi ya mtoto wa kike kusoma kwa malengo Balozi Seif  ameagiza Wazazi wowote watakaohusika na kitendo cha kuwaozesha  Watoto wao wa Kike wakati wanasoma Uongozi wa Serikali ya Mkoa usimamie katika kuona Vyombo vya Dola vinawachukulia hatua za Kisheria mara moja Wazazi hao ikiwa ni pamoja na kuwaweka ndani.
“ Jamii inahitaji kuwa na Ewataalamu wa Kike ambao watahusika kushughulikia huduma zinazofanywa na Wanaume Kitaalamu ambazo hazistahiki kutokana na Tamaduni na Imani wa Kidini”. Alisisitiza Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alionya kwamba tabia hii inayoonekana kuendelea kwa baadhi ya Mitaa Nchini inarejesha nyuma maendeleo ya Mtoto wa kike aliyekandamizwa kwa muda mrefu kutokana na mfume Dume uliozoeleka kwa kipindi kirefu kilichopita.
 Balozi Seif akimchum Mtoto Sulhia Ali wa Kijiji cha Mwambe huku Mama yake Mzazi akitabasamu mara baada ya kusalimiana na Wananchi wa Kijiji hicho alipofika kukagua maendeleo ya ujenzi wa Skuli ya Sekondari.
 Mhandisi wa Ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Wara Ali Khamis Shaibu akimpatia maelezo Balozi Seif kuhusu ujenzi wa majengo ya Skuli hiyo unaokwenda kwa wakati uliopangwa.
Naibu Katibu Mkuu Wikzara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Maalim Abdulla Mzee Abdulla akiteta na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  kwenye majengo ya Skuli Mpoya ya Sekondari inayojengwa katika Kijiji cha Wara Chake Chake Pemba.
Balozi Seif akikagua baadhi ya Majengo ya Nyumba za Makaazi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar zinazojengwa katika eneo la Pagali Wilaya ya Chake chake Pemba.
Umma wa Wananchi wa Kijiji cha Mwambe waliokuwa wakisikiliza nasaha za Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hayupo pichani alipofika kukagua Mradi wa Ujenzi wa Skuli ya Sekondari kwenye eneo hilo.


Hivyo makala Makamu wa Pili wa Rais wa Zanziubar Balozi Seif Ali Iddi akaguwa Majengo mapya ya Skuli za Sekondari

yaani makala yote Makamu wa Pili wa Rais wa Zanziubar Balozi Seif Ali Iddi akaguwa Majengo mapya ya Skuli za Sekondari Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Makamu wa Pili wa Rais wa Zanziubar Balozi Seif Ali Iddi akaguwa Majengo mapya ya Skuli za Sekondari mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/makamu-wa-pili-wa-rais-wa-zanziubar.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Makamu wa Pili wa Rais wa Zanziubar Balozi Seif Ali Iddi akaguwa Majengo mapya ya Skuli za Sekondari"

Post a Comment