MAHAKAMA YATAKA AKINA HANSPOPPE WAONDOLEWE.

MAHAKAMA YATAKA AKINA HANSPOPPE WAONDOLEWE. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAHAKAMA YATAKA AKINA HANSPOPPE WAONDOLEWE., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAHAKAMA YATAKA AKINA HANSPOPPE WAONDOLEWE.
kiungo : MAHAKAMA YATAKA AKINA HANSPOPPE WAONDOLEWE.

soma pia


MAHAKAMA YATAKA AKINA HANSPOPPE WAONDOLEWE.


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa siku saba kwa upande wa mashitaka kukamilisha mchakato wa kubadilisha hati ya mashitaka ili kuwaondoa washitakiwa Zacharia Hanspoppe na Franklin Lauwo kwenye kesi ya utakatishaji fedha inayowakabili Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na makamu wake.
Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai kudai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba washitakiwa Aveva na makamu wake, Godgrey Nyange `Kaburu’ wapo mahakamani hapo isipokuwa washitakiwa hao wawili.
Wakili Swai alidai kuwa mara ya mwisho mahakama ilitoa amri ya kuwaondoa Mwenyekiti wa Usajili wa Klabu ya Simba, Hanspoppe na Lauwo katika hati ya mashitaka ili kesi iweze kuendelea kwa washitakiwa wawili ambao ni Aveva na Nyange.
Alidai kuwa walifanya utaratibu wa kupeleka jalada la kesi hiyo kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) na kwamba katika ufuatiliaji wake, amebaini kuwa DPP bado hajalishughulikia suala hilo kwa kuwa yupo nje ya Mkoa wa Dar es Salaam.
‘’Hivyo tunaomba tupewe wiki mbili kuhakikisha DPP analifanyia kazi hata kama atakuwa Dodoma ama Dar es Salaam tutamfuata huko huko,’’ alidai Swai.
Hata hivyo, mshitakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Aveva aliomba mahakama iwape muda wa siku saba kwa sababu siku 14 ni nyingi na kueleza kuwa kitendo cha upande wa mashitaka kuendelea kuchelewesha jambo hilo, kinawaumiza.
Kwa upande wa Nyange, yeye alidai kuwa suala la kubadilisha hati ya mashitaka kwa kuwaondoa washitakiwa hao wawili, ni la muda wa zaidi ya miezi miwili licha ya kwamba wanajua kuwa wapo mahabusu kwa zaidi ya mwaka mmoja na kuendelea kukaa huko ni changamoto.
Pia alidai kuwa kuendelea kuwapatia upande wa mashitaka wiki mbili ni kuendelea kuwafi cha katika gereza la Keko bila sababu za msingi. Baada ya kusikiliza hoja hizo, Hakimu Simba alihoji upande wa mashitaka kuona malalamiko ya washitakiwa kama hayana msingi, ambapo walijibu kuwa yana msingi.
Hakimu Simba alisema kuwa anatoa siku saba kwa sababu mshitakiwa Aveva anahudhuria kliniki kila wiki na kuwataka wahakikishe kuwa wanakamilisha taratibu hizo kwa sababu wao ndio wanachelewesha kesi hiyo na kueleza kuwa kama hawaitaki, waifute.
Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 17, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Awali, mawakili wa utetezi wakiongozwa na Nehemia Nkoko, Nestory Wandiba na Evodius Mtawala uliwasilisha maombi yao kwa kuhoji kwamba haikuwa sahihi kwa mahakama kupokea hati ya mashitaka wakati washitakiwa wawili hawakuwepo mahakamani.
Hata hivyo, hoja hiyo ilipingwa na Wakili Swai akidai kuwa mahakama ilishakubali hati hiyo ya mashitaka na wasihtakiwa waliopo waliweza kusomewa na kuamriwa kesi itasikilizwa baada ya washitakiwa wengine kupatikana.
Washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka 10 yakiwemo ya kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi, kutoa maelezo ya uongo na utakatishaji fedha haramu. Chanzo: habari leo.


Hivyo makala MAHAKAMA YATAKA AKINA HANSPOPPE WAONDOLEWE.

yaani makala yote MAHAKAMA YATAKA AKINA HANSPOPPE WAONDOLEWE. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAHAKAMA YATAKA AKINA HANSPOPPE WAONDOLEWE. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/mahakama-yataka-akina-hanspoppe.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAHAKAMA YATAKA AKINA HANSPOPPE WAONDOLEWE."

Post a Comment