MAHAKAMA JUMUISHI MBEYA KUSOGEZA HUDUMA ZA KIBENKI NDANI YA MAHAKAMA HIYO

MAHAKAMA JUMUISHI MBEYA KUSOGEZA HUDUMA ZA KIBENKI NDANI YA MAHAKAMA HIYO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAHAKAMA JUMUISHI MBEYA KUSOGEZA HUDUMA ZA KIBENKI NDANI YA MAHAKAMA HIYO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAHAKAMA JUMUISHI MBEYA KUSOGEZA HUDUMA ZA KIBENKI NDANI YA MAHAKAMA HIYO
kiungo : MAHAKAMA JUMUISHI MBEYA KUSOGEZA HUDUMA ZA KIBENKI NDANI YA MAHAKAMA HIYO

soma pia


MAHAKAMA JUMUISHI MBEYA KUSOGEZA HUDUMA ZA KIBENKI NDANI YA MAHAKAMA HIYO

Viongozi wa Mahakama Kanda ya Mbeya (kushoto) wakiwa katika majadiliano na Viongozi wa Benki ya NMB, majadiliano juu ya uanzishwaji wa huduma za kibenki ili kuwarahishia wateja wanaofika katika Mahakama hiyo.
Mjumbe kutoka NMB akichangia jambo katika majadiliano.
Picha ya pamoja baada ya majadiliano, (wa pili kushoto) ni Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya.
              (Picha na Rajabu Singana, Mahakama Kuu, Mbeya)   

Na Rajabu Singana. Mahakama Kuu Mbeya
JAJI Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Mhe. Robert Makaramba amekutana na uongozi wa benki ya NMB na kufanya mazungumzo juu ya uanzishwaji wa huduma za Kibenki katika jengo la Mahakama Kuu Mbeya linalotoa huduma kwa Mahakama Kuu, Mahakama ya Hakimu Mkazi na Mahakama ya Wilaya.

Mhe. Makaramba alikutana na uongozi huo mapema Agosti 28, aliwaeleza viongozi wa NMB kwamba Mahakama ipo katika maboresho makubwa ya huduma zake kupitia mpango mkakati wa miaka mitano (2015-2020) unaolenga kumsogezea mwananchi huduma.

Kutokana na changamoto ya kufanya malipo ambayo wamekuwa wakiipata wananchi Mhe. Makaramba aliwaomba NMB kusogeza huduma zao katika jengo la Mahakama Kuu Mbeya. 

Akichangia katika mazungumzo hayo, Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Straton Chilongola alisema kwa sasa Benki ya NMB imekuwa ikifanya kazi kwa kushirikiana na Mawakala ambao hufanya kazi za Kibenki. 

Bw. Chilongola aliongeza kwa kusema kwamba watafanya utaratibu wa kuanzisha ‘Cash Collection Point’ kwa ajili ya wananchi kufanya malipo ya Huduma za Mahakama. 

Meneja wa Wakala wa Benki wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Bw. Respicious Denis aliongeza kuwa kwa sasa benki ya NMB imekuwa ikifanya vizuri kwa kutumia Mawakala kwenye malipo na makusanyo mbalimbali ambapo tayari baadhi ya taasisi za serikali zinatumia huduma hiyo. 

Alizitaja taasisi hizo ni paoja na TRA, Idara ya Maji Mbeya na walitumia mfumo huo katika makusanyo ya NaneNane mwaka huu.

Ifahamike kwamba baada ya ukarabati mkubwa wa jengo la Mahakama Kuu Mbeya, Uongozi wa Mahakama ya Tanzania ulifikia maamuzi ya kulifanya jengo hii kuwa Kituo Jumuishi cha kutoa huduma za Mahakama. 

Wadau muhimu wa Mahakama walipatiwa ofisi za kuendeshea shughuli zao ikiwa ni njia mojawapo ya kumsogezea mwananchi huduma na kuondoa usumbufu kwa wananchi. Wadau walipotiwa ofisi ni pamoja na Mawakili wa Kujitegemea, Mawakili wa Serikali, Polisi na Huduma kwa Jamii. 

Pamoja na mambo mengine viongozi hawa wameafikiana kuanzisha Huduma za Kibenki wiki ijayo kwa kumtumia Wakala wa Benki.


Hivyo makala MAHAKAMA JUMUISHI MBEYA KUSOGEZA HUDUMA ZA KIBENKI NDANI YA MAHAKAMA HIYO

yaani makala yote MAHAKAMA JUMUISHI MBEYA KUSOGEZA HUDUMA ZA KIBENKI NDANI YA MAHAKAMA HIYO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAHAKAMA JUMUISHI MBEYA KUSOGEZA HUDUMA ZA KIBENKI NDANI YA MAHAKAMA HIYO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/mahakama-jumuishi-mbeya-kusogeza-huduma_30.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MAHAKAMA JUMUISHI MBEYA KUSOGEZA HUDUMA ZA KIBENKI NDANI YA MAHAKAMA HIYO"

Post a Comment