title : Kikwete amjulia hali Dkt. Kigwangalla kitengo cha mifupa MOI
kiungo : Kikwete amjulia hali Dkt. Kigwangalla kitengo cha mifupa MOI
Kikwete amjulia hali Dkt. Kigwangalla kitengo cha mifupa MOI
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Hamisi Kigwangalla kitengo cha mifupa MOI anapopatiwa matibabu. Kulia ni Mke wa Waziri Dk Kigwangalla, Dkt. Bayoum Awadhi Kigwangalla.
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Andrew Chale ambaye ni Mwandishi wa Habari Maalum wa Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Hamisi Kigwangalla. Kulia ni Dkt. Bayoum Awadhi Kigwangalla mke wa Waziri Dkt.Kigwangalla.
Na Andrew Chale, Dar
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete jioni ya tarehe 14,
Agosti 2018 amemtembelea na kumjulia hali Waziri wa
Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla aliyelazwa
katika wodi maalum kitengo cha Taasisi ya mifupa
MOI, hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Hii inakuwa ni mara ya pili kwa Kikwete kumtembelea Dk
Kigwangalla ambapo awali alimtembelea Agosti
8, alipokuwa amelazwa Wodi ya Mwaisela akipatiwa
Matibabu ya awali.
Kikwete amemtakia kila lakheri katika kipindi hiki kwa
kuuguza majeraha ya mkono na sehemu za mwili ikiwemo
mbavu ambazo kwa sasa hali yake inaendelea kuimarika kwa
majibu wa Madaktari wa kitengo hicho cha mifupa MOI.
Awali tokea kufanyiwa operesheni ya mkono ameweza
kufanya mazoezi taratibu ikiwemo kutembea mwenyewe
katika viunga hivyo vya Muhimbili.
Dkt. Kigwangalla alipata ajali ya gari mnamo Agosti 4, 2018
huko Manyara akiwa katika ziara ya kikazi ambapo katika
ajali hiyo iliyokuwa na watu 6, watano walijeruhiwa na
mmoja alifariki dunia ambaye alikuwa afisa habari
mwandamizi wa Wizara hiyo, Hamza Temba.
Hivyo makala Kikwete amjulia hali Dkt. Kigwangalla kitengo cha mifupa MOI
yaani makala yote Kikwete amjulia hali Dkt. Kigwangalla kitengo cha mifupa MOI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Kikwete amjulia hali Dkt. Kigwangalla kitengo cha mifupa MOI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/kikwete-amjulia-hali-dkt-kigwangalla.html
0 Response to "Kikwete amjulia hali Dkt. Kigwangalla kitengo cha mifupa MOI"
Post a Comment