HIZI HAPA SABABU ZILIZOMFANYA MTATIRO KUNG'OKA CUF

HIZI HAPA SABABU ZILIZOMFANYA MTATIRO KUNG'OKA CUF - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa HIZI HAPA SABABU ZILIZOMFANYA MTATIRO KUNG'OKA CUF, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : HIZI HAPA SABABU ZILIZOMFANYA MTATIRO KUNG'OKA CUF
kiungo : HIZI HAPA SABABU ZILIZOMFANYA MTATIRO KUNG'OKA CUF

soma pia


HIZI HAPA SABABU ZILIZOMFANYA MTATIRO KUNG'OKA CUF

Kanda wa Chama cha Wananchi (CUF) Julius Mtatiro akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaaam.

Mwambawahabari
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.

Aliyekuwa Mwenyekiti ya Kamati ya Uongozi Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro ametangaza kujivua uanachama wa Chama hicho na kutangaza kujiunga na Chama Mapinduzi (CCM)

Akizungumza na waandishi wa habari leo  jijini Dar es Salaam Mtatiro amesema kuwa ameamua kuchukua uamuzi huo kwa kuwa jukwaa alilokuwa analisimamia katika siasa kwa miaka kumi limeshindwa kumpa nafasi yakuifanyie nchi yake maendeleo.

Mtatiro amesema kuwa ataendelea  kuwatumikia watanzania pamoja na kupambana na umasikini popote atakapokwenda.

"Uamuzi huu sio kwa ajili ya kutafua cheo ila nimefanya hivyo ili kutimiza malengo yangu ya kulitumikia taifa pamoja na kuwa balozi mzuri wa nchi yangu popote nitakapo kuwa" amesema Mtatiro.

Amefafanua kuwa kabla ya kufikia  maamuzi hayo alitafakari kwa muda wa mwezi mmoja kuhusu mchango wake kama kiongozi katika kuliletea taifa  maendeleo.

Amesema kuwa baada ya kutafakari  na kuchukua maamuzi ya kujitoa katika Chama cha Wananchi (CUF) amebaini mambo kadhaa ambayo yamekuwa sababu kuu ya kujitoa katika chama hicho.

Mambo hayo ni pamoja na mgogoro wa  ndani wa Chama cha CUF,  ushiriki wake kama kijana katika uongozi na kuleta maendeleo katika taifa pamoja na mustakabali wake wa siasa.

"Nimekuwa mwanachama na kiongozi ndani ya CUF kwa muda wa miaka kumi, lakini nimeona mchango wangu ni mdogo sana katika kuliletea taifa la Tanzania maendeleo" amesema Mtatiro.

Amesema kuwa sasa atafanya siasa za vitendo kwa ajili ya kumsaidia Rais Dkt. John Magufuli katika kufanikisha mipango mbalimbali ya kimaendeleo.

Mtatiro amesema kuwa ajenda nyingi zikiwemo elimu bure, ufisadi, rushwa ambazo zipo ndani ya CUF zinatekelezwa Chama cha CCM.


"Sioni sababu ya kuendelea kuwa CUF wakati yote tuliokuwa tunayazungumza sasa yanafanyiwa kazi kikamilifu" amesema Mtatiro.


Hivyo makala HIZI HAPA SABABU ZILIZOMFANYA MTATIRO KUNG'OKA CUF

yaani makala yote HIZI HAPA SABABU ZILIZOMFANYA MTATIRO KUNG'OKA CUF Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala HIZI HAPA SABABU ZILIZOMFANYA MTATIRO KUNG'OKA CUF mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/hizi-hapa-sababu-zilizomfanya-mtatiro.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "HIZI HAPA SABABU ZILIZOMFANYA MTATIRO KUNG'OKA CUF"

Post a Comment