AL MUNTAZIR SEMINARI YAWAKUTANISHA WANAFUNZI BARANI AFRIKA NCHINI

AL MUNTAZIR SEMINARI YAWAKUTANISHA WANAFUNZI BARANI AFRIKA NCHINI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa AL MUNTAZIR SEMINARI YAWAKUTANISHA WANAFUNZI BARANI AFRIKA NCHINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : AL MUNTAZIR SEMINARI YAWAKUTANISHA WANAFUNZI BARANI AFRIKA NCHINI
kiungo : AL MUNTAZIR SEMINARI YAWAKUTANISHA WANAFUNZI BARANI AFRIKA NCHINI

soma pia


AL MUNTAZIR SEMINARI YAWAKUTANISHA WANAFUNZI BARANI AFRIKA NCHINI

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

SHULE ya sekondari ya Seminari ya Kiislamu Al Muntazir kwa mara nyingine tena wamewakutanisha wanafunzi wa shule za Sekondari nchini na nje ya nchi kwa lengo la kufanya mashindano ya kujadili mada mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

Mjadala huo umepewa jina la "Mwalimu Nyerere Schools Invitational Debate Championships" ili kuwajenga na kuwaandaa wanafunzi hao kuwa wataalamu na wajuzi kwa miaka ijayo.Akizungumza na vyombo vya habari Mkuu wa shule ya Al Muntazir Reuben Kimani ameeleza kuwa mashindano hayo kwa shule za Sekondari na hiyo ni mara ya tatu yamefanyika yakihusisha washiriki zaidi ya 200.

Na hiyo ni kwa lengo la kuwafanya wawe na fikra pana kwa elimu ya chuo watakayoendelea nayo, ambapo ameeleza kuna shule kutoka Zimbabwe na Kenya na wenyeji Tanzania wakiwakilishwa na shule za Tusiime, Shaaban Robert, shule ya wavulana na wasichana Feza, Aghakan na wenyeji Al Muntazir.

Aidha ameeleza kuwa mashindano hayo yatachukua siku 3 wale watakaofanya vizuri watatunukiwa vyeti na watashiriki mdahalo mkubwa utakaofanyika Desemba mwaka huu nchini Botswana. Kuhusiana na maandalizi kwa wanafunzi wao Kimani ameeleza kuwa wametoa mafunzo kwa wiki mbili yakihusisha utafiti hivyo hawana shida kwa shindano hilo na amewataka wanafunzi kuja kujishiriki kwa kutazama na kupata uzoefu kutoka kwa wanafunzi kutoka barani Afrika.

Mwalimu na mlezi wa klabu ya Lugha ya kiingereza kutoka Al Muntazir Seminari Bi. Getrude Mtenga akieleza namna shule yao ilivyojipanga katika kukabiliana na mashindano hayo.
Mkuu wa shule ya Sekondari ya Seminari ya Al Muntazir, Reuben Kimani akitoa neno kwa washiriki kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.
Baadhi ya wanafunzi walioshiriki mdahalo huo kutoka shule za sekondari nchini.
Wanafunzi kutoka Zimbabwe (wenye suti za bluu) wakisikiliza mjadala uliokuwa unaendelea.KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>


Hivyo makala AL MUNTAZIR SEMINARI YAWAKUTANISHA WANAFUNZI BARANI AFRIKA NCHINI

yaani makala yote AL MUNTAZIR SEMINARI YAWAKUTANISHA WANAFUNZI BARANI AFRIKA NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala AL MUNTAZIR SEMINARI YAWAKUTANISHA WANAFUNZI BARANI AFRIKA NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/al-muntazir-seminari-yawakutanisha.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "AL MUNTAZIR SEMINARI YAWAKUTANISHA WANAFUNZI BARANI AFRIKA NCHINI"

Post a Comment