title : ZANZIBAR 24 WATOA MSAADA WA CHAKULA KWA SOBA HOUSE YA DESTROIT YA MCHINA MWANZO
kiungo : ZANZIBAR 24 WATOA MSAADA WA CHAKULA KWA SOBA HOUSE YA DESTROIT YA MCHINA MWANZO
ZANZIBAR 24 WATOA MSAADA WA CHAKULA KWA SOBA HOUSE YA DESTROIT YA MCHINA MWANZO
Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar
Waathirika wa dawa za kulevya wanaoishi katika nyumba ya kurekebisha tabia (Soba House) ya Detroit iliyoko Kwamchina mwanzo wameiomba Serikali kuendeleza mapambano ya kupiga vita uingizaji na utumiaji wa dawa hizo nchini.
Vijana hao walitoa ombi hilo baada ya kupokea msaada wa chakula uliotolewa na Mtandao wa Kijamii Zanzibar 24 ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya kutimia miaka mitatu tokea kuanzishwa mtandao huo.
Kijana Alawi Abdalla anaeishi nyumba hiyo alisema ikiwa Serikali haitaongeza nguvu za kuwatafuta na kuwakamata waingizaji wakubwa wa dawa za kulevya vijana wengi wataendelea kuathirika.
Aliwashauri vijana ambao bado hawajaanza kutumia dawa za kulevya wasijaribu kuzionja kwani sio kitu cha kuonja na nihatari kwa usalama wa afya zao.
Alawi aliishauri Serikali kuwatafutia msaada wa nyenzo za kufanyia kazi vijana waliopita Soba House na kufanikiwa kurekebisha tabia zao ili watakapo rejea katika jamii waweze kujitegemea.
Mtendaji Mkuu wa Zanzibar 24 Suleiman Juma Is-haka akimkabidhi Mkuu wa Soba House ya Detroit Rashid Kassim msaada wa chakula katika hafla iliyofanyika katika nyumba hiyo iliyopo Kwamchina mwanzo.
Baadhi ya vijana wanaoishi nyumba ya kurekebisha tabia ya Detroit iliopo kwa Mchina mwanzo wakifuatilia kukabidhiwa msaada wa chakula uliotolewa na Mtandao wa Kijamii wa Zanzibar 24.
Mkuu wa Soba House ya Detroit Rashid Kassim akitoa shukrani zake mbele ya waandishi wa habari wa Zanzibar 24 baada ya kupokea msaada wa chakula katika hafla iliyofanyika kwenye nyumba hiyo Kwamchina mwanzao.
Mmoja wa vijana wanaoishi nyumba ya kurekebisha tabia ya Detroit Alawi Abdalla akizungumza na waandishi wa habari wa Zanzibar 24 Amina Omar (kulia) na Fat-hiya Shehe katika hafla iliyofanyika Kwamchina mwanzao. Picha na Ramadhani Ali Maelezo Zanzibar.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala ZANZIBAR 24 WATOA MSAADA WA CHAKULA KWA SOBA HOUSE YA DESTROIT YA MCHINA MWANZO
yaani makala yote ZANZIBAR 24 WATOA MSAADA WA CHAKULA KWA SOBA HOUSE YA DESTROIT YA MCHINA MWANZO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ZANZIBAR 24 WATOA MSAADA WA CHAKULA KWA SOBA HOUSE YA DESTROIT YA MCHINA MWANZO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/zanzibar-24-watoa-msaada-wa-chakula-kwa.html
0 Response to "ZANZIBAR 24 WATOA MSAADA WA CHAKULA KWA SOBA HOUSE YA DESTROIT YA MCHINA MWANZO"
Post a Comment