WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA KUCHAMBUA PAMBA CHA GAKI

WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA KUCHAMBUA PAMBA CHA GAKI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA KUCHAMBUA PAMBA CHA GAKI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA KUCHAMBUA PAMBA CHA GAKI
kiungo : WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA KUCHAMBUA PAMBA CHA GAKI

soma pia


WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA KUCHAMBUA PAMBA CHA GAKI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha kuchambua pamba cha GAKI na kusema amevutiwa na uwekezaji uliofanywa na wamiliki wa kiwanda hicho ambao ni Watanzania.

“Ninawapongeza wazawa walioamua kujenga kiwanda hiki kwa sababu viwanda kama hivi vinasaidia kukuza kilimo hapa nchini, kiwanda hiki kinachambua pamba na kusindika mafuta,” alisema.

Ametoa pongezi hizo jana jioni (Ijumaa, Julai 13, 2018) wakati akizungumza na wafanyakazi wa kampuni ya GAKI Investment pamoja na wananchi waliofika kumsikiliza mara baada ya kukagua utendaji kazi wa kiwanda hicho kilichopo Manispaa ya Shinyanga.

Waziri Mkuu alisema amevutiwa na ujenzi wa kiwanda hicho kwa sababu kinatoa uhakika wa soko la pamba ikizingatiwa kwamba mikoa yote inayolima zao hilo, mwaka huu imezalisha pamba kwa wingi kuliko kawaida.

“Mwitikio wa wakulima wa zao la pamba unaonyesha kwamba bado wana imani na Serikali yao na ndiyo maana nimewaonya wajumbe wa bodi ya SHIRECU kuwa wajihoji kama kweli wameomba nafasi hizo ili kuwatumikia wananchi,” alisema.

“Msije mkadhani kuwa SHIRECU ni mahali pa kuganga njaa. La hasha! Ni mahali pa kukuza soko la pamba. Tunataka viongozi wa sasa watambue kuwa hawajaenda SHIRECU ili kushiba, lazima walete mabadiliko kwenye ushirika na kama hawawezi waachie ngazi,” alisisitiza.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mitambo ya kuchambua pamba wakati alipotembelea kiwanda cha kuchambua pamba cha Gaki Invesiment cha mjini Shinyanga, Julai 13, 2018. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack na watatu kulia ni Mkurugenzi Mtendanji , Gaspar Kileo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama pamba inayosubiri kuchambuliwa wakati aliootembelea kiwanda cha kuchambua pamba cha Gaki kilichopo mjini Shinyanga Julai 13, 2018. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack na watatu kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda, Gaspar Kileo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mbengu za pamba wakati alipotembelea kiwanda cha kuchambua pamba cha Gaki Investment kilichopo mjini Shinyanga Julai 13, 2018. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack na kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda hicho, Gaspar Kileo.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu


Hivyo makala WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA KUCHAMBUA PAMBA CHA GAKI

yaani makala yote WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA KUCHAMBUA PAMBA CHA GAKI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA KUCHAMBUA PAMBA CHA GAKI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/waziri-mkuu-majaliwa-atembelea-kiwanda.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA KUCHAMBUA PAMBA CHA GAKI"

Post a Comment