title : WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMKABIDHI DKT TIZEBA MATREKTA 500 YA URSUS
kiungo : WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMKABIDHI DKT TIZEBA MATREKTA 500 YA URSUS
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMKABIDHI DKT TIZEBA MATREKTA 500 YA URSUS
Na Mathias Canal, Dar es salaam
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) leo 4 Julai 2018 amemkabidhi Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba jumla ya matrekta 500 yatakayopelekwa kwa vyama vya ushirika vya msingi ili wakulima kunufaika na tija katika kilimo hususani zao la Pamba.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika wakati wa uzinduzi wa maonesho ya 42 ya sabasaba katika viwanja vya Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam, Mhe. Dkt Tizeba alisema kuwa sekta ya kilimo nchini bado inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo tija ndogo inayosababishwa na matumizi madogo ya pembejeo, huduma duni za ugani na matumizi ya zana duni za kilimo ambapo wakulima wengi wanatumia majembe ya mkono au kutumia maksai wakati wa kulima.
“Katika kilimo cha Pamba msimu wa mwaka 2017/2018 ushahidi unaonyesha kwamba wakulima walichelewa kuanza kuandaa mashamba yao kwa sababu Maksai wakati wa kiangazi wanadhoofu sana, na mara mvua inaponyesha hawawezi kulima mpaka majani yawe mengi ndio wapate nguvu za kuanza kulima, hali hii inaondoa uwezekano wa wakulima kutumia teknolojia mpya katika kilimo kama vile kilimo hifadhi ambacho kimedhihirika kuongeza tija zaidi ya mara mbili” Alikaririwa Mhe Dkt. Tizeba
Aliitaja mikoa itakayoanza kunufaika na mpango huo katika awamu hii ya kwanza kuwa ni pamoja na Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Tabora na Geita, awamu ya pili ikijumuisha mikoa ya Singida, Kagera, na Kigoma huku awamu ya tatu ikitarajiwa kuhusisha mikoa ya Kanda ya Mashariki kwa kuzingatia ongezeko la uzalishaji wa pamba katika maeneo hayo.
Mhe Tizeba alisema mtazamo wa mpango huo ni kuunganisha nguvu za mkulima mmoja mmoja ili kuharakisha kuleta maendeleo yao ambapo utatekelezwa kwa kutumia sehemu ya fedha zinazolipwa AMCOS kama kamisheni ya kusimamia ununuzi wa pamba ambapo matarajio ni kukusanya Bilioni 6 kama uzalishaji wa pamba utafika kilo milioni 400 kwa mwaka.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim M. Majaliwa (Mb) akimkabidhi hati ya makabidhiano Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba ya matrekta 500 yaliyonunuliwa na wadau mbalimbali wa kilimo nchini katika maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 4, 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe ikiwa ni ishara ya kukabidhi matrekta 560 yaliyonunuliwa na wadau mbalimbali wa kilimo nchini katika maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 4, 2018. Watatu kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara ya Uwekezaji, Charles Mwijage, Wapili kulia ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba na kulia ni Naibu Waziri wake, Dkt, Mary Mwanjelwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Waziri wa kilimo Dkt Charles Tizeba Kitabu cha Mwongozo wa Taratibu za Kujenga Kiwanda Nchini Tanzania baada ya kufungua Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 4, 2018.
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba (Mwenye maiki) akizungumza kabla ya kukabidhiwa matrekta 500 yaliyonunuliwa na wadau mbalimbali wa kilimo nchini katika maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 4, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe ikiwa ni ishra ya kukabidhi matrekta 560 yaliyonunuliwa na wadau mbalimbali wa kilimo nchini katika maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 4, 2018. Watatu kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara ya Uwekezaji, Charles Mwijage na kushoto ni Naibu Waziri wake, Mhandishi Stella Manyanya. Wapili kulia ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba na kulia ni Naibu Waziri wake, Dkt, Mary Mwanjelwa
Hivyo makala WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMKABIDHI DKT TIZEBA MATREKTA 500 YA URSUS
yaani makala yote WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMKABIDHI DKT TIZEBA MATREKTA 500 YA URSUS Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMKABIDHI DKT TIZEBA MATREKTA 500 YA URSUS mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/waziri-mkuu-kassim-majaliwa-amkabidhi.html
0 Response to "WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMKABIDHI DKT TIZEBA MATREKTA 500 YA URSUS"
Post a Comment