WAZIRI MKUU ATOA SIKU 14 WAJASIRIAMALI WAHAME

WAZIRI MKUU ATOA SIKU 14 WAJASIRIAMALI WAHAME - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI MKUU ATOA SIKU 14 WAJASIRIAMALI WAHAME, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI MKUU ATOA SIKU 14 WAJASIRIAMALI WAHAME
kiungo : WAZIRI MKUU ATOA SIKU 14 WAJASIRIAMALI WAHAME

soma pia


WAZIRI MKUU ATOA SIKU 14 WAJASIRIAMALI WAHAME

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Taifa Kahama, Julai 15, 2018
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ngoma wakati  alipowasili kwenye Uwanja wa Taifa Kahama   kuhutubia mkutano wa hadhara, Julai 15, 2018. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
………………..

*Ni baada ya kukagua eneo la viwanda vidogo na kupewa malalamiko
  
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kahama Mji, Bw. Anderson Msumba ahakikishe ndani ya siku 14 anawahamisha wajasiriamali wote waliogoma kuhamia eneo la viwanda la Bukondamoyo.

“Wauza mbao, wachomeaji grili, wenye gereji wote, hakuna ruhusa kuendelea kubakia mjini wakati tumewapa eneo la bure la ekari 500. Lile eneo ni zuri kwa biashara lakini kuna watu wamegoma kuhamia kule. Mkurugenzi hakikisha wote hawa wanahamia kule mara moja na atakayekiuka, akamatwe,” alisema.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana (Jumapili, Julai 15, 2018) wakati akizungumza na wajasiriamali wachache waliohamia kwenye eneo la viwanda la Bukondamoyo katika kata ya Zongomela, wilayani Kahama mkoani Shinyanga mara baada ya kulikagua.

“Ninawaagiza wajasiriamali wote walioko mjini wawe wamehamia huku ifikapo tarehe 30 Julai, 2018. Mkuu wa Mkoa ikifika tarehe moja Agosti, wewe njoo na Kamati yako ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na mkiwakuta huko mjini, wakamateni na kuwaweka ndani,” alisema.

Alimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kahama Mji aimarishe barabara za eneo hilo kwa sababu kuna magari yanatakiwa kupeleka mizigo lakini pia kuna magari ya wateja yatapaswa kwenda huko kwa hiyo ni lazima pafikike kwa urahisi.

“Tengeneza barabara, weka taa za barabarani za solar, lakini pia uangalie uwezekano wa kuweka kituo kidogo cha polisi kwa sababu kuna kundi kubwa la wafanyabiashara na wateja. Pia wekeni zahanati ili hawa wakipata majeraha, wahudumiwe kwa haraka,” alisema.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wajasiriamali wawili, Bw. Haji Selemani na Bw. Sudi ambao walisema wajasiriamali wote walipewa agizo la kuhamia eneo la viwanda lakini kuna wenzao wamegoma, na wanaendelea kufanya biashara mjini ambako kuna wateja wengi.

Akizungumza na maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Taifa wa Kahama, Waziri Mkuu alirudia kutoa agizo hilo na kuwaahidi kwamba watapatiwa mafunzo ya uwezeshaji na taasisi iliyoko kwenye ofisi yake ifikapo Julai 30, mwaka huu.

“Ifikapo Julai 30, atakuja Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) hapa Kahama na kutoa mafunzo ya namna ya kupata mikopo na kufanya biashara. Haya mafunzo yatatolewa kulekule, kwa hiyo wahini kuhamia mpate kushiriki fursa hiyo,” alisema.

Wakati huohuo, Mkurugenzi wa Mji wa Kahama, Bw. Anderson Msumba alisema eneo hilo la viwanda lina ukubwa wa ekari 500 na lilipimwa na kugawanywa kisha vikapatikana viwanja 678 vyenye ukubwa wa kati, wa chini na wa juu (high, medium and low density).

“Viwanja hivyo wamepewa bure isipokuwa wanapaswa kulipia gharama za kupata hati ambazo zinaanzia sh. 150,000 hadi 300,000 kutegemeana na ukubwa wa kiwanja. Maji yapo ila yataongezwa mradi wa Zongomelo ukikamilika.”

Kuhusu barabara za eneo hilo, Bw. Msumba alisema TARURA walishatoa makadirio yao ambayo ni sh. bilioni 1.3 na wameshapeleka maombi hayo TAMISEMI. Alisema maeneo kwa ajili ya ujenzi wa kituo kidogo cha polisi pamoja na mabenki, yameshatengwa, ni suala la wahusika kwenda kuomba.



Hivyo makala WAZIRI MKUU ATOA SIKU 14 WAJASIRIAMALI WAHAME

yaani makala yote WAZIRI MKUU ATOA SIKU 14 WAJASIRIAMALI WAHAME Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU ATOA SIKU 14 WAJASIRIAMALI WAHAME mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/waziri-mkuu-atoa-siku-14-wajasiriamali.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAZIRI MKUU ATOA SIKU 14 WAJASIRIAMALI WAHAME"

Post a Comment